Mkuu wa Kituo cha Reli cha Dar es salaam Bi. Rose Ngauga akizungumza na mwandishi wetu aliyemtembea ofisini kwake kujua mawili matatu kuhusiana na usafiri huo. WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, wamefurahia kuanza kwa usafiri wa treni waliousubiri kwa muda mrefu ulioanza juzi.
Abiria wakigombea kupanda treni kutoka katikati ya jiji kueleke Ubungo.
Kamera yetu leo ilitua katika ofisi ya mkuu wa kituo kinachodili na usafiri huo, Bi. Rose Ngauga na kuzungumza mambo kadhaa kuhusiana na usafiri huo. Ngauga alisema kuwa usafiri huo siyo nguvu ya soda kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na kwamba utakuwa endelevu.

Wanafunzi wakipanda katika behewa lao maalumu tayari kwa safari.
Bi. Rose akimuonyesha mwandishi wetu (hayupo pichani) tiketi zinazotumika kwa abiria wa kawaida na wanafunzi.
Abiria wakiwa katika dirisha la kukatia tiketi.
Wanafunzi wakikata tiketi katika dirisha maalumu kwa ajili yao.
Kichwa cha treni kikiunganishwa na mabehewa kabla ya kuanza safari.
Abiria wakiwa wameketi ndani ya behewa wakisubiri kuanza safari.
Mkuu wa Kituo cha Reli cha Dar es salaam  Bi. Rose Ngauga akikagua mabehewa kabla ya gari moshi kuanza safari leo saa 9.40 alasiri.
...akikabidhiwa ripoti.
Gari moshi likiwa katika mwendo na baadhi ya abiria wakionekana wakichati na simu.
Mwandishi mwanadamizi wa Global Publisher, Haruni Sanchawa akishuka kutoka katika treni hiyo maeneo ya Ubungo Maziwa ambako treni hiyo umalizia safari yake.
Abiria wakishuka kwenye treni.
Pamoja na usafiri huo kuanza, mafundi wa shirika la reli bado wanaendelea na ukarabati wa reli kama wanavyoonekana pichani.
(HABARI PICHA : Haruni Sanchawa / GPL)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hii ni solution nzuri sana. Foleni na hajari za barabarani zitapungua.
    Haya ni maendeleo mazuri Tanzania. I am so happy to hear this.

    ReplyDelete
  2. Naomba kujua hii treni inapitia vituo gani na mwisho ni kituo gani??? Je usafikiri huu unagaharimu kiasi gani??

    ReplyDelete
  3. Jessy........Hajari ni kitu gani!??

    ReplyDelete
  4. Ivi hii tabia chafu ambayo ipo tanzania tu ya kupigana vikumbo wakati wa kuingia ndani ya chombo cha usafiri itakwisha lini? ukiangalia vizuri hizo picha abiria wakiwa ndani kila mtu amekaa lakini huko nje walikua wanapigana vikumbo, Natamani ningekua na sauti ya kuwataka kupanga foleni kwa kila usafiri uwe binasfi au wa umma lengo ni kuwafunza tabia nzuri na uvumilivu, yaani tunashindwa hata na majerani zetu (kenya)wao upanga foleni hata kwenye hiace.Sijui nani anaweza nisemea hili kwa wabongo inaniuma sana hasa kwa hii picha mbaya tunayoionesha.

    ReplyDelete
  5. sasa uzinduzi wa usafiri wa treni uendane na elimu kwa jamii Tustaarabike tuwe kama hapo jirani tu Kenya maana Ulaya mbali, tupange foleni kuingia na iwe ndio utaratibu mambo ya kugombea ya kishamba. Tuelimishane hata kwa njia ya video ikibidi, tuoneshwe wenzetu wafanyavyo ktk vyombo vya umma

    ReplyDelete
  6. this is good idea ila kwa upande wa ticket ili kupunguza msongamano wa watu shirika lingejaribu kutengeneza ticket za wiki nzima kama mtu akinunua tiket moja anajua anaitumia 5days na iwe na rangi tofauti na ticket nyingine hata kwa wanafunzi itawasaidia pia.sijajua nauli ni kiasi gani

    ReplyDelete
  7. Wahusika tafadhali wekeni utaratibu/sheria ya kupanga foleni badala ya kusukumana. Huu ni wakati muafaka wa sisi Watanzania kubadilika

    ReplyDelete
  8. WATANZANIA, WAKAZI WA DAR, BABA MHESHIMIWA MWAKYEMBE, ANKO MICHUZI HONGERENI.
    HII NI HATUA MUHIMU SANA KWA MAENDELEO YA JIJI NA VITONGOJI VYAKE.
    KAMA ALIVYOSEMA MDAU HAPO JUU, TRENI ZITAPUNGUZA AJALI BARABARANI, VURUGU ZA MAKONDA KUPIGA WANAFUNZI, UCHELEWAJI SHULENI/KAZINI, USAFIRISHAJI MIZIGO {LIKIWEKWA BEHEWA LA MIZIGO} N.K ILI KUFANYA USAFIRI HUU UWE ENDELEVU TUFANYAJE?
    1.TUTUNZE MALI NA KUTOKUHUJUMU MALI ZA TAZARA NA UMMA KWA UJUMLA. KILA MMOJA WETU AWE MLINZI WA USAFIRI HUU KUHAKIKISHA RELI HAZIVURUGWI ILI KUEPUSHA AJALI
    2. WANANCHI/ WASAFIRI TULIPE NAULI SAHIHI NA TUACHE UJANJA UJANJA. TUNATAKA TRENI UWE MRADI ENDELEVU? BASI TUUTUNZE.
    4.MHESHIMIWA NA WIZARA, HAKIKISHENI KUNA MATENGENEZO YA TRENI NA RELI ANGALAU MARA MOJA KILA MIEZI SITA. MNAFUNGA RELI WIKI KADHAA KUCHEKI KILA KITU SHWARI.
    3.HILI NI JAMBO JEMA. SIO LA CCM WALA CHADEMA, NI LA WATANZANIA, TUSHIRIKIANE KUMPA MOYO MHESHIMIWA MWAKYEMBE, HUYU NI KIONGOZI WA SHOKA. TUSITIE UCHAMA KWENYE HILI. VIONGOZI WA UPINZANI PANDENI TRENI NA MUMPONGEZE MWAKYEMBE MSITAFUTE MAKOSA KWENYE HUDUMA YA JAMII, SI MNATETEA HAKI ZA RAIA WOTE?
    4. MHESHIMIWA MWAKYEMBE, KILA LA HERI. UONGOZI NI VITENDO SIO MANENO. ASANTE BABA. AIKA MBE MKUU

    ReplyDelete
  9. Nyie wakazi wa Dar ebu kuweni wastaaratbu hiyo treni siyo daladala,pangeni foleni ndiyo ustaarabu sehemu nyingine duniani.TRL elimisheni abiria wapande kwa mstari.

    ReplyDelete
  10. Pamoja na kuleta huduma ya usafiri wa treni ambao ni WAJIBU wa serikali, vile vile izingatie kujenga platforms au sehemu za kupandia abiria katika kila kituo. Kufanya hivyo kutasaidia watoto, wazee, walemavu na wote ambao hawatajiweza kupanda ngazi hizo kama ilivyo sasa.

    ReplyDelete
  11. Hongera sana nchi yangu Tanzania kwa hatua kubwa iliyofikiwa kwa upande wa usafiri wa abiria wa Dar es Salaam. Hii itawawezesha wanafunzi kufika shuleni na majumbani mapema hali kadhalika wafanyakazi na wote ambao watatumia usafiri huu. Kitu ambacho naomba wahusika wakiangalie ni upangaji foleni wakati wa kukata tiketi na kuingia kwenye treni. Yaani inatakiwa tuwe wastaarabu katika hili tuachane na kutumia mabavu kwani hali hii ishapitwa na wakati. Uongozi wa TRL naomba waliangalie hili kwa karibu. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  12. hii ni hatua nzuri ya maendeleo kwa nchi yetu ya tanzania..huduma hii iboreshwe zaidi na ipanuliwe zaidi kama mwisho wa siku iweze kufika sehemu zote za jiji..hongereni wizara husika..tuunge mkono juhudi hizi na tusianze kuzitafutia kasoro zisizo na maana....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...