Ubao wa Matokeo unavyoonekana baada ya kumalizika kwa Dakika tisini za Mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya Simba na Yanga uliochezwa usiku wa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Yanga,Said Bahanuzi akiwatoka mabeki wa timu ya Simba alipoingia kwenye lango la timu hiyo wakati wa mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya Simba na Yanga uliochezwa usiku wa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.
Didier Kavumbagu wa Yanga akiangalia nani wa kumpatia pasi mbele ya Mabeki wa timu ya Simba wakati wa mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya Simba na Yanga uliochezwa usiku wa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.
.....Hatari langoni mwa timu ya Simbaaa......
Refarii wa mchezo wa huo,Mathew Akrama akitoa kadi nyekundu wa Mchezaji wa Yanga,Simon Msuva (27) baada ya kumchezea rafu Beki wa timu ya Simba,Juma Nyoso (24) alielala chini wakati wa mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya Simba na Yanga uliochezwa usiku wa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lao la kusawazisha.
Kipa wa timu ya Simba,Juma Kaseja akiruka juu kudaka mpira uliokuwa ukielekea langoni kwake katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya Simba na Yanga uliochezwa usiku wa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 1-1.









Mpiga picha wa YANGA utamuona tu, kwahiyo yeye alikaa huku kwa SIMBA tu kutegemea ndio kutafungwa, matokeo yake ameshindwa ku balance story na kufanya kana kwamba SIMBA ndio walikuwa wakishambuliwa bila wao kushambulia hata mara moja
ReplyDeleteSHAME on you / AIBU hiyo mpiga picha
Mnyama alipiga mpira ambao Yebo hawakutegemea, wale vijana wadogo, christopher, Mkude na Ngalema pamoja na Dumayo na Msuva wa Yanga ni hatari sana na tegemeo ktk soka la bongo. Mwamuzi pia alijitahidi kiasi chake ingawa kulikuwa na makosa kwa pande zote ambayo aliyaachia.
ReplyDeleteYANGA IMESHINDWA KUNG'ARA MBELE YANGA?...
ReplyDelete1.Mtoa Maoni wa kwanza kama Mpiga Picha ni wa Yanga sasa mtoa hii Kichwa cha Habari ni Simba!
2.Bao la Matokeo limekosewa na hayo ni makosa ya Kitekinolojia kwa vile sasa mabao sio ya Chaki kama Kipindi kile zamani kwa sasa ni ya Elektroniki, lilitakiwa kama lionekane hivi:
YANGA S.C -1936
SIMBA S.C -0
NA SIO
YANGA S.C-1
SIMBA S.C-1
Inatakiwa TFF walipeleke Bao la Mtokeo nje kwa matengenezo kutokana na makosa ya kiufundi kama haya lilivyosoma matokeo ya jana usiku!
3.Kama Msimbazi wangetufunga YANGA mabao kama yale ya Kimipango ya Netiboli, ile 5-0 tena?,,,Kwa kweli nilijiandaa kula ugali mkubwa wa Kilo 3 na maharage huku nikishushia na maziwa na mgando ili leo niweze KUNYA mchana saa 7.30 kati kati ya barabara Mtaa wa Msimbazi!
Wewe Mwana Msimbazi mtoa Maoni wa Kwanza ulifikiri mtapata tena mvua ya mabao kama yake eee?
ReplyDeleteUnaota ubwabwa wa juzi?
Jana Makande makavu yenye maharage magumu yasiyoiva!
Mdau wa kwanza Anony Thu Oct 04, 08:41:00 AM 2012 acha unazi wa Msimbazi !
ReplyDeleteJana tuliwashika Idara zote, angalia kama muda ungekuwa zaidi ya pale filimbi ilipopulizwa kwa hata dk 10 mbele, tungezamisha la pili baada ya kuwachomolea la kwanza!
Kila jamaa waki chomoka Bendera juu,,,!, hata katikati ya uwanja kuna kuzidi?
Si uliona?
Jana tumethibitisha Msimbazi mna mipango sana!
ReplyDeleteIlikuwa almanusura mnyama ale kisu gizani!
Lilichomolewa kwa matuta, sema na hilo ili kauli ikamilike.
ReplyDeleteKwani tuta sio goli? mbona zile tano tatu ni za matuta? Messi anafunga 30 na 10 ni za matuta. Hamkosi cha kusema!
ReplyDeleteMdau wa nane Anonymous wa Fri Oct 05, 02:17:00 AM 2012 NI UKWELI UMENENA KUTOKANA DHARAU YA HUYO MWANA MSIMBAZI WA SABA (7) HAPO Thu Oct 04, 03:06:00 PM 2012
ReplyDelete.....Lilichomolewa kwa matuta, sema na hilo ili kauli ikamilike.
(Pia mkumbuke ya kuwa ile ni adhabu imezaliwa na Mchezaji wa Simba kushika, hatari ambayo ingezaa Goli wavuni kwa Kaseja!, sasa hii mbona huongelei?)
TUNATHIBITISHA HAPA KWA KAULI YAKE NI KUWA MARA ZOTE MKATAA MUME AU MDAI TALAKA HANA SABABU!