Kuna dada mmoja anasoma chuo fulani Buguruni na pia ni mfanyakazi hivyo jioni akitoka kazini ndipo huenda shule.Sasa akiwa njiani kuelekea chuo akapigiwa simu na mtu asiyemfahamu akajitambulisha kwamba yeye ni daktari wa Lugalo hosp.
na kumuulizia habari za mwanae ambae alishawahi kwenda kumtibu pale na chakushangaza zaidi akataja mpaka aina na rangi ya nguo aliyovaa siku ile alipokwenda hapo hospitali na yote yalikuwa kweli.
Na zaidi akamwambia najua sasa hivi unaelekea chuo Buguruni na kweli ilikuwa hivyo, lakini mwishoni akamweleza kwamba kuna mambo anataka kujua kuhusu hicho chuo hivyo nae anaelekea huko hivyo akifika tu atamtafuta. Kwa muda wote huo huyo dada hakuweza kabisa kumkumbuka ila akajipa moyo kwamba yamkini huyo mtu atakuwa anamfahamu vizuri.
Baada ya kutoka chuo akiwa na wenzake watatu akawa anawasimulia habari za huyo mtu ndipo simu yake ikaita,kupokea yule mtu akamwambia nakuona uko na wenzio wawili mnavuka barabara na kumueleza jinsi alivyovaa sasa wenzie wakasema huyo mtu anakufahamu haiwezekani hapa tupo watatu kweli na ameweza kukutambua. Kisha huyo mtu akamwelekeza mahali alipo ambapo haikuwa mbali na barabara.
Lakini alipomtazama hakumfahamu kabisa, basi akampa mkono kumsalimia, baada ya hapo hakujitambua na zaidi alijikuta yuko maeneo ya chuo kikuu cha DSM akiwa hoi.
Kuangalia simu na kila kitu chake kilikuwa salama na hakufanyiwa kitu chochote, kwa bahati kulikuwa kuna ndugu yake anasoma chuo hivyo akawasiliana nae ili kupata msaada ikabidi awahishwe Mwananyamala hosp. lakini ikaonekana sumu iliyotumika ni kali na dawa yake wanayo Regency hosp,hivyo akawahishwa Regency na kupata matibabu.
Baada ya ufahamu kumrudia akakuta mtu huyo kachukua pesa zote kwenye mpesa,tigo pesa na benki ( NMB na CRDB) kiasi cha milioni 3, hivyo inawezekana walipompa sumu alitaja password pasipo kujijua.
Na benki walipotazama kwenye ATM Camera waliona picha ya huyo mtu na yeye alimkumbuka vizuri, lakini polisi Kijitonyama wakakiri kwamba kesi hizo sasa hivi zimetokea mara nyingi na huo mtandao ni mkubwa, walipoenda kwenye usajili wa simu walikuta ni huyo huyo na jina lake ndilo alilojitambulisha.Ingawa polisi wameshindwa kumkamata.
Akiwa kituo cha polisi mara huyo mtu akampigia simu akimwambia ‘’kumbe wewe ni muoga sana tutakurudishia pesa zako’’. Sasa kumbe wanachofanya wanakuambia’’ tutafutie mtu ambae unahisi ana pesa kuliko hizi halafu tukifanikiwa tutarudisha pesa zako’’ hivyo inawezekana nae kuna mtu anaemjua alifanyiwa hivyo akaamua kumtaja yeye.
HIVYO NI KUOMBA MUNGU NA KUWA WAANGALIFU


ReplyDeleteUSIMPE MKONO MTU USIYEMJUA, KUSALIMIANA SIYO LAZIMA KUPEANA MIKONO.
Wizi huu sisi tuliwatangazia, ninyi bado mnapeana mikono na watu msio wajua, JE hamkuamuni tulivyo waambia?
ReplyDeletePole sana dada. Mungu akufariji na hongera kwa ujasiri wa kutupa hizi habari najua ni ngumu. Na mimi nina rafiki yangu alipata mkasa unaofanana July 2012!!
ReplyDeleteKama polisi wanazo picha, nafikiri kungeazishwa kipindi cha television cha kuwatambua wahalifu wanaotafutwa na picha zao zipo tayari polisi! wawekwe kwenye Tv na magazeti ili kupunguza uhalifu huo! Mie nina wasiwasi na hawa watu wa mitandao ya simu pia. Maana hakuna data protection tanzania. Na wanaweka detail zetu zote za tunapoisshi na kadhalika. Huu uhalifu umeanza sambamba na kuzishwa kwa kuandikisha mobile phones! Ndio maana wenzetu Data protection Act!! Watanzania tuamke!!
POLE NA ASANTE KWA TAARIFA,HII INAWEZA KUMPATA MTU YOYETE.KWA KUWA HAWAKUFANYIA `CHOCHOTE` SHUKURU MUNGU,PESA UTAPATA ZINGINE.HAWA HAWAHITAJI KUKUFANYIA CHOCHOTE,HAWA WASHENZI SHIDA YAO PESA TU
ReplyDeleteMbona haieleeweki? Kama anaweza kufuatilia kila kitu mpaka kwenda kuripoti polisi mimi naona itakuwa ni mfanyakazi wa benki au polisi.
ReplyDeleteYa Allah awaokoe na kuwaepusha na mabalaa kama hayo. POLISI VIPI KAMA WAMEONA VIDEO YA HUYO MTU NA ALIYETENDEWA KAMUONA NA MA TV KIBAO YA NCHINI YAPO VIPI WANASHINDWA KUIONYESHA KWENYE TV MAALUMU MWIZI HUYU ANATAFUTWA KWA MIEZI TU TUONE KAMA WATAENDELEA HII YOTE AJIRA HAKUNA AU SIJUI USALAMA SIO MZURI TUNATAKIWA KUWA MAKINI HATA MAUSAFIRI MA TAX WAONYESHE ID SASA NDIO DEREVA WA TAX? PIA NIMESIKIA ZA TAX DADA ZETU WANAVYOUMIZWA. POLISI HATUNA AMANI NAO PIA.
ReplyDeleteit does not make sense, hizi ndio story za changamsha balaza - kama ni kweli je kwa nini polisi watume picha hiyo magazetini, redioni, kwenye televisheni na kutangaza vituo vyote vya polisi kuwa huyo mtu anatafutwa? hizo CCTV kwenye ATM zimewekwa kwa ajili ya kuwakamata waarifu sio video ya kuangalia tu. polisi hawezi kuwa wanasema tu kuwa hii imeshawatokea watu wengi bila kufanya lolote, yaani tumefikia pabaya hivyo? ushauri wangu huyo dada awape jina la polisi kwa kushirikiana na polisi, hao watu wampigie polisi kanzu (under polisi) wamkamate huyo jamaa sio tunaongea ongea tu. wangine tunajisifu kuwa tulishasema hili lakini hamkusikiliza.
ReplyDeleteNadhani kama alivyoandika anonym mmoja hapo juu,imefikia wakati mwafaka kwa polisi kuanzisha kipindi maalum katika television cha kuonyesha wahalifu.Kazi ya kamera ni kutambua wahalifu hivyo ni vizuri kuwaonyesha katika television ili wanaowafahamu wawasaidie polisi katika kutoa taarifa.Hii itasaidia sana kupunguza uhalifu kwani hata nchi za ulaya hutumia njia hii.
ReplyDeleteSeven-Denmark
WATANZANI TUPO MBELE KITECHNOLOGIA BWANA!!!!!
ReplyDeleteNasikitika na sitasema mengi kwani mke wangu alipanda taxi kwenda bank wakati anatoka ATM yule taxi driver akamnunulia soda na hapo ndio kosa alilofanya.basi pesa yote ktk ATM ikatolewa. Nasikitika police nilipeleka picha na hakuna hata moja hadi leo lililofanyika.nasikia ni mtandao wa Wa Nigeria na waTanzania
ReplyDelete
ReplyDeleteHii kazi wangepewa USALAMA WA TAIFA, mtandao wao mkubwa pia ingetumika kama changamoto kwenye masomo yao kimatendo.
Matukio yanazidi, yanapuuzwa tu, mpaka ifikie beyond repair ndio tuamke??!!!
NINI FAIDA YA HIZO CAMERA BASI
ReplyDelete"walipoenda kwenye usajili wa simu walikuta ni huyo huyo na jina lake ndilo alilojitambulisha.Ingawa polisi wameshindwa kumkamata."
-???????!!!!!!!!!!, KAMATA MBWEHA HUYO, KESHAPATIKANA HANA PA KUKIMBILIA UNLESS NI KAMTANDAO.
ALAFU MNASEMA HUKUMU YA KIFO IONDOLEWE KWELI?WAJUA HIYO SUMU ALIYOPEWA IMESHAATHIRI KIASI GANI VIUNGO VYA MWILI WAKE NA KUPUNGUZA MDA WAKE WA KUISHI?TUSIANGALIE KWAKUA YU MZIMA ANAONGEA TU.HAWA WATU WASAKWE NA WAONESHWE KTK TV ZOTE NA KUPEWA ADHABU KALI KWA KUFANYA HIVYO TUTAKOMESHA KISHA BAADA YA KUDILI NA HAWA WANAOFUATA NI WEZI WA KUVUNJA VIOO VYA MAGARI KWA KUTUMIA KEMIKALI NA VILE VILE WAKIPATIKANA ONESHA KTK TV KISHA ADHABU KALI.
ReplyDelete
ReplyDeleteAisee my fellow Tanzanians hio ni kitu inaitwa Niger Boys a.k.a Yahoo Boys from Nigeria mbona hvyo vitu vimetokea sana hata ile scam ya kutumia Tigo Pesa ni wao wame introduce chezea wanigeria weweee
wamebarikiwa akili ya kufikiri balaa na wana chop money oohhh
nakumbuka nilipo fika chuo mwezi wa 9 nilikaa nao nyumba moja wakawa wakiniambia michezo wanayofanya nigeria sumu aliyopewa hata sio uchawi bali in inhaled gas
pole sana dada Mungu atakusaidia utapata hela nyingine jasho la mtu alihibiwa hata siku moja
ReplyDeleteHapa mtapiga kelele wee lakini no any action itachukuliwa police wenyewe woote ni wale wajinga wa mwisho na wana njaaa balaa usitegemee
kuna msaada hapa
Nimecheka, eti Taxi driver akamnunulia mke wako soda, ni lazima huyo mke is fresh from kijijini. Toka lini dreva taxi akamnunulia abiria soda? Labda walikuwa na yao mengine
ReplyDelete