Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni watengenezaji wa kilaji cha Konyagi,David Mgwasa 'Mpambanaji'  (wa tatu kulia) akikabidhi sehemu ya vifaa vya Muziki kwa viongozi wa Bendi ya Muziki wa Dansi nchini ya Msondo Ngoma (Baba ya Muziki) vilivyotolewa na Kampuni yake kwa ajili ya kuuendeleza muziki wa Dansi hapa nchini.Makabidhiano haya yamefanyika jioni ya leo katika Viwanja vya Leaders,Kinondoni jijini Dar es salaam.Wengine Pichani toka kulia ni Meneja Mauzo TDL,Joseph Chibehe,Meneja wa Konyagi, Martha Bangu,Maalim Muhidin Gurumo,Said Mabela a.k.a Daktari,Roman Mng'ande na Shaaban Dede ambao ni wanamuziki wa Msondo Ngoma Band.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni watengenezaji wa kinyaji cha Konyagi,David Mgwasa (kulia) akikabidhi gitaa kwa Mwanamuziki Mkongwe wa Bendi ya Msondo Ngoma,Mzee Said Mabela (kushoto) ikiwa ni sehemu ya vifaa vya muziki vilivyotolewa na Konyagi kwa bendi hiyo,jijini Dar es Salaam jioni ya leo.Katikati ni Kiongozi wa Bendi hiyo,Maalim Muhidin Gurumo.
Wanamuziki wa Bendi ya Msondo Ngoma wakiwa kwenye picha ya Pamoja na viongozi wakuu wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Ltd ambao ni watengenezaji wa kilaji cha Konyagi mara baada ya kukabidhiwa vifaa vipya vya Muziki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hivi ndivyo ilivyokuwa bendi zetu zinapewa ufadhili iwe kutoka kwa makampuni,taasisi za umma na binafsi au mfadhili mmoja mmoja kama Hugo Kisima n.k

    Si bure muziki za dansi wa Kamanyola bila jasho, Masantula ngoma ya mpwita, Sikinde, Msondo, Afrosa, Sokomoko, Saboso, Njeje n.k ziliweza kutawala muziki Afrika mashariki na kati.

    Pongezi kwa Konyagi kuonesha mfano na siyo kusapoti tu wafokaji wa maiki wanaotumia CD.

    Mdau
    Muziki wa Dansi.

    ReplyDelete
  2. Pongezi sana watengenezaji wa Konyagi
    kwa mchango huu mkubwa,nyinyi mmefungua njia kwa wahisani wengine nao wachangie Muziki wa dansi ni uhai wa muziki wa Tanzania.
    Wadau
    FFU

    ReplyDelete
  3. NI HATUA YA NZURI NA YA KUPONGEZWA SANA.
    SWALI KWA MENEJA WA BENDI VIONGOZI NA MASENETA, MBONA TUNAKARIBIA KUMALIZA MIAKA MIWILI BILA ALBAM? AU NDO TAYARI NA NYIE MMSHAKUWA KAMA WALE WENZENU WALEE, MUNATUNYIMA RAHA MASHABIKI nA WAPENZI WENU TUSIOKUWA NA FURSA YA KUJA KWENYE MAONESHO YENU, NAOMBA MULIFIKIRIE SANA HILO.
    SWALI LA PILI MBONA MUMEUTELEKEZA UKUMBI WENU WA MBAGALA? KWA NINI MUSITAFUTE MTU WA KUUENDESHA HATA KAMA NI kWA SHEREHE ZA KITCHEN PARTY?

    ReplyDelete
  4. Bwana Michuzi fikisha pongezi zangu kwa Konyaji kwa hatua yao hii muhimu ya kuuweka hai muziki wa dansi Tanzania. Natoa wito kwa makampuni mengine yaige mfano huu.

    ReplyDelete
  5. Hongera Konyagi !

    Muwe na mwenendo huo huo wa Udhamini zaidi ya Vifaa vyaKazi (Muziki) hata ikifikia ktk vipindi vya Wanamuziki kuugua Hospitalini mchangie kutoa msaada wa matibabu pia!

    ReplyDelete
  6. Bendi zingine je?

    Au ndio kusema Msondo na Wapenzi wao ndio wanywaji wazuri wa Konyagi?

    Vipi kwa Mtani wenu wa Jadi Kigogo Mbuyuni kwenye 'Konyagi-B' a.k.a Gongo mmetoa chochote?

    ReplyDelete
  7. Sasa wajameni nyie Wazee wa Msondo Sheikh Said na Maalim ni muda wa kustaafu na kurejea Misikitini!

    ReplyDelete
  8. Swalaaaaa, Swalaaaaa, Swalaaaaaa !

    Msondo Ngoma Swalaaaaaaaa!

    Maalim Muhidin na Sheikh Said Swalaaaaaa !

    Sasa hivi ni Saa 11 kasoro Dakika 7 Alfajiri amkeni tujiandae Kuswali!

    Swalaa ni Bora kuliko Starehe!

    ReplyDelete
  9. Utu uzima dawa mngebakia kuwa Washauri wa Muziki mkiwa Mikekani Majumbani badala ya kukaa Jukwaani hadi lala salama!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...