Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 15 kutoka kwa Waziri Barnabas Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya NMB, kama mchango wa benki hiyo kwa ajili ya kununulia madawati ya shule za msingi katika mkoa huo, Ikiwa ni mchango wa benki hiyo katika maendeleo ya elimu Mkoani Katavi, Mkoa wa Katavi umezinduliwa leo na Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda, na kuhudhuriwa na wananchi wengi wa mkoa huo.
Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na wafanyakazi wa benki ya NMB wakati alipotembelea banda la benki hiyo katika maonyesho yaliyofanyika wakati wa uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi mjini Mpanda.Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) akiteta jambo na Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda, wakati wa kutathmini mrejesho wa kongamano la Uwekezaji katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika uliofanyika Oktoba 17 mwaka jana mjini Mpanda. Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe akikaribisha wageni mbalimbali waliofika kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano hilo na Mkoa wa Katavi lililofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Maji Mjini Mpanda hivi karibuni.
Waziri Mkuu wa Mizengo Pinda akimshukuru Domina Feruzi, Meneja Mwandamizi wa NMB anayeshughulikia biashara za Serikali, mara baada ya kupokea hundi hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa mkoa wa Katavi, katikati ni Lucresia Makiriye, Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za juu Kusini.
Wananchi wakitembelea moja ya Banda ya wawekezaji wa kigeni wakati wa maonyesho hayo ya uzinduzi wa mkoa wa Katavi uliofanyika leo mjini Mpanda.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bw. Paza Mwamlima akitoa utaratibu wakati wa Kongamano la Tathmini ya Mkutano wa Uwekezaji Ukanda wa Ziwa Tanganyika lililofanyika sambamba na uzinduzi wa mkoa wa Katavi kuanzia juzi na kumalizika jana mjini Mpanda huku uzinduzi wa mkoa huo ukifanyika leo.
Baadhi ya maofisa mbalimbali wa Serikali waliohudhuria katika Kongamano hilo lililofanyika mjini Mpanda mkoa mpya wa Katavi.
Mabalozi kutoka nchi mbalimbali walihudhuria kongamano hilo zikiwemo Burundi, Misri Zambia, Japan na DRC Congo hapa wakifuatilia Mada katika kongamano hilo. Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akikaribishwa na Lucresia Makiriye, Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za juu Kusini, katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na Benki ya NMB kwa ajili ya Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kwenye hoteli ya Lyamba lya Mfipa mjini Mpanda
Wafanyakazi wa benki ya NMB wakijumuika katika picha ya pamoja mara baada ya kula Chakula cha jioni na wakuu wa Mikoa na wilaya kwenye hoteli ya Lyamba Lya Mfipa mjini Mpanda.
Maofisa mbalimbali wa benki ya NMB kutoka makao makuu , Mbeya na Mpanda wakiwa katika picha ya pamoja wakati benki hiyo ilipoandaa chakula cha jioni kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya kwenye hoteli ya Lyamba Lya Mfipa mjini Mpanda jana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...