Watuhumiwa wa kesi ya Mauaji ya Marehemu Swetu Fundikira,wakiwa Mahakamani mchana wa leo kabla ya kusomewa hukumu yao.

Kwa taarifa za uhakika  zilizoifikia Globu ya jami,kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania,zinaeleza kuwa hukumu ya kesi ya mauaji ya Marehemu Swetu Fundikira inayowakabili askari jeshi Sajent Rhoda Robert, Koplo Ally Ngumbe na Mohamed Rashidi imetolewa mchana huu na kwamba wote wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Washtakiwa hao watatu wanadaiwa kuwa siku ya Jumamosi tarehe 23 Januari, 2010 walimpiga bila huruma Swetu Fundikira katika maeneo ya Kinondoni katika makutano ya barabara  za Mwinjuma na Kawawa jijini Dar es salaam mpaka kusababisha kifo chake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. HUKUMU YA KUNYONGA INATAKIWA IFUTWE JAMANI! WENZENU WAJERUMANI NA WAINGERZA. WALIOTULETEA HUKUMU HII! HAWAITUMII KWAO!
    WANGEHUKUMIWA MAISHA TU HAO ILI WAJUTIE MAKOSA YAO YA KUUA! KUKAA JELA BILA KUTOKA.

    ReplyDelete
  2. Aliyeuwa kwa upanga atakufa kwa upanga. R.I.P Swetu hatimae haki imetendeka .

    ReplyDelete
  3. Ni Kweli hukumu za kifo zimepitwa na wakati, kwanza zinahisiwa zina gharama zaidi.

    ReplyDelete
  4. Nina kubaliana na Anonymous kwamba wakati umefika Hukumu ya Kunyonga inatakiwa ifutwe.Iko wapi sauti ya civil instutions kuhusu sheria ya kunonga nchini? Watu wana hitaji kuelimishwa.

    ReplyDelete
  5. Juzi gazeti moja limeandika taarifa za mfungwa aliehukumiwa miaka 15 jela kwa kosa la kukutwa na SMG mwaka 2010 amekutwa mtaani na SMG nyingine hahahahaha watu wanajiuliza kapenyaje mageti yote,kwa jinsi tanzania yetu ilivyo kubuhu kwa rushwa waweza wafunga maisha ikawa jina tu wamefungwa maisha kumbe watafichwa mbali na upeo wa waliowatendea mabaya.

    ReplyDelete
  6. I hope mchangiaji wa kwanza atakua na mawazo hayo ya kufuta hiyo hukumu hata siku akiuawa baba yake,kaka yake au yoyote katika familia yake.

    ReplyDelete
  7. No complain, justice have been done we have to remember that these three individuals killed someone who was loved by his family and according to the court it has been proved beyond reasonable doubt that they did it, Ain't say that they deserve it, personally i hate capital punishment and nobody deserve to die this way but we are the country of laws. Let us be lead by laws then we can say that we are living in a civil society. Some states in United States are either fighting to re-instate or put to an end to the capital punishment but Europe have done away with it for a long time now that is their businesse , hopeful in our coming new constitution this issue will be addressed based on people's opinions and am glad that people have been involved on airing out their opinions, until then let's us follow our existing laws.

    ReplyDelete
  8. They should have known better than to take another life... I am not for the death penalty but I don't think I am totally against it either. An eye for an eye. May the victim R.I.P and may they rot in hell...

    ReplyDelete
  9. Mchangiaji wa kwanza hujui, Marekani ni moja ya nchi zinazoongoza kwa kunyonga duniani!. Kawaulize Texas.

    Hatuwezi kuishi kwenye nchi ambayo watu hawajali sheria, wanakuwa kama wanyama kuua watu wasio na hatia bure!. Mtu hamumjui, mnampiga mpaka anakufa bila sababu, hii ndio nchi tunayoitaka?

    Wanastahili kunyongwa!

    ReplyDelete

  10. Jino kwa jino, jicho kwa jicho, shingo kwa shingo.

    No more no less.

    ***Anon wa NOV 20th 11:41:00 PM SUMMED IT ALL

    ReplyDelete
  11. UNAJUA KILA MTU ANA MTAZAMO WAKE BINAFSI!
    AMERIKA UNAYOISEMA WEWE ASILIMIA TISINI WANAONYONGWA, NI WATU WA ASILI YA AFRIKA!
    HUKUMU YA KUNYONGA IMEPITWA NA WAKATI.
    HATA ANGEUWAWA BABA YANGU AU MAMA YANGU.
    MSIMAMO WANGU UNGEKUWA NI HUO NILIOTOA MWANZO, SWETU FUNDIKIRA, ALIKUWA NDUGU YETU NA RAFIKI YETU MPENDWA, LAKINI WANGEHUKUMIWA MAISHA INGEKUWA VEMA ZAIDI ILI WAJUTIE MAKOSA YAO! MJERUMANI ALIKUWA ANANYONGA WATU ZAMANI WAKATI ANATUTAWALA, ALIPOONDOKA ALIMUACHIA MWINGEREZA SHERIA HIYO YA KUNYONGA.
    LAKINI KWA SABABU WAO WANAWAPENDA ZAIDI WANANCHI WAO WALIIFUTA SHERIA HII YA UKATILI.
    KWANINI SISI TUENDELEE KUITUMIA?
    ANGALIA SADAM HUSSEIN, ALINYONGWA NA AMERIKA WAKATI ALIKUWA HANA MAKOSA ILA ANGEKUWEPO LEO KAMA SI SHERIA HII MBAYA ANGEACHIWA HURU.
    HUO NI MFANO MDOGO SANA NDUGU ZANGU.

    ReplyDelete
  12. UUMINI LALA SALAMA ?

    WAKATI MNAFANYA UZINZI HAMKUWA WALA MNASWALI, BAADA YA MAUAJI MMEKUWA WASWALIHINA TENA BAADA YA KUWEKWA LUPANGO!

    ReplyDelete
  13. Hatuhukumu !

    Isipokuwa mmetuangusha, inaonyesha hapo kabla hamkuwa Waumini kwa kuwa mlikuwa mnafanya Uzinzi, huko Kuswali mmeaqnza wakati mkiwa Mahabusu.

    ReplyDelete

  14. Tuseme yoooote, ALIYEUA ikithibitika KAUWA naye AUWAWE!

    Hakuna cha kupitwa na wakati hapa.

    Hao "wanaowapenda" wananchi wao minchi inawashinda, no ethics, no morals, nothing! eti ndio maendeleo.

    Sheria si ipo? Si imethibitika wameuwa? Go for the jugular!

    ReplyDelete
  15. Hamna haja ya kulalama kuhusu hukumu ya kifo, maana Maraisi wetu kuanzia Nyerere mpaka Kikwete hawasaini hiyo hukumu. Nyerere alikuwa akiisaini tu pale ambapo umetishia siasa zake, kama ile ya Mwamwindi.

    Mnayesema waumini wakati wako lupango, wenzenu ndiyo wamepewa second chance hivyo, na wakitubu Mwenyezi Mungu anaweza kuwasamehe. Ikiwa mnajituma kustawisha swala na kutenda mema, Mwenyezi Mungu awazidishie, lakini kujiona ninyi ni bora kuliko wengine katika imani ni mapungufu. Hujafa hujaumbika, au hamjui?

    ReplyDelete
  16. Thu Nov 22, 02:07:00 AM 2012


    Mdau unaemalizia ...Hujafa hujaumbika, au hamjui?

    Ilitakiwa wafanye Uumini tokea kabla ya haya huenda Mwenyezi angewaongoza wasifikwe na balaa hili.

    Sasa unataka kusema nini hapa, yaani mtu ufanye maasi kama vile hakuna Mungu halafu leo yamekukuta ndio tena unamgeukia Mungu ?

    ReplyDelete
  17. Mdauwa wa Thu Nov 22, 02:07:00 AM 2012

    ...Mnayesema waumini wakati wako lupango...

    Second chance ina aina yake ya Makosa siyo kama haya waliyofanya hawa jamaa (MAUWAJI+UZINZI)...MENGINE ZAIDI WALIYOFANYA ANAYAJUA MWENYEZI... tunatakiwa tuishi kwa tabia njema na kufuata Kanuni na Misingi ya Dini ktk maisha yetu yote, pia ni Uraiani na sio Lupango!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...