Wachezaji wa timu ya mpira wa pete wa timu ya Bunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (waliovaa nyeusi) wakicheza na timu ya chuo cha Ufundi cha Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid timu ya Bunge iliibuka mshindi kwa mabao 24 -13
Timu ya mpira wa pete wa timu ya Bunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (waliovaa nyeusi) wakicheza mpira na timu ya chuo cha Ufundi cha Arusha
Timu ya bunge la jumuiya ya afrika mashariki ikipewa mawaidha na kocha wake Rashid wakati wa mapunziko
Picha na habari na Woinde Shizza
wa Globu ya Jamii
Timu ya Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Bunge sports club) imeweka kambi ya wiki mbili Jijini Arusha kwa ajili ya mashindano kombe la Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayo timua vumbi jijini Nairobi nchini Kenya.
Mwenyekiti timu hiyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kinondoni Idd Azan alisema kuwa pamoja na majukumu waliyonayo bado wana nafasi kubwa ya kushiriki miashindano hayo na kuhakiksha kuwa kombe hilo linarudi Tanzania.
Azan alisema kuwa lengo la michuano hiyo ni kushirikiana na wabunge wa nchi nyingine zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kudumisha umoja na kuwa na mshikamano kupitia michezo.
Aidha alieleza kuwa lengo lingine ni kudumisha ushirikiano wa Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuwapa burudani wananchi wa nchi zinazounda Jumuiya husika.
‘’Timu yetu ipo katika hali nzuri na tayari tumeshafanya marekebisho ya makosa tuiyofanya kipindi cha nyuma hivyo watanzania watarajie ushindi kwa kuwa wachezaji wote wapo katika hali nzuri.”alisema Azan
Katika michezo ya kujipima nguvu, timu ya mpira wa pete ya wabunge imeichapa timu ya arusha technical magoli 24-13 katika mtinange uliochezwa katika dimba la Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Katika mtanange mwingine timu ya mpira wa pete ya Ngorongoro creater imechapwa magoli 42-31 na timu ya Mpira wa pete ya Bunge jijini Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...