Hayati Mhashamu Aloysius Balina |
Imeandikwa na
Emmanuel Makene
Wapendwa Wana wa Shinyanga;
UTANGULIZI
Kifo cha Mhashamu Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga,
Mhashamu Aloysius Balina, aliyefariki dunia
katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza siku ya Jumanne 06 Novemba 2012; kimeacha pengo kubwa kwa Kanisa
Katoloki Tanzania .
Askofu Balina amefariki akiwa amebakiza siku 10 tu afikishe miaka 15 kamili kama Askofu wa Jimbo la Shinyanga. Alikuwa ni Askofu wa
tatu wa Jimbo la Shinyanga na wa kwanza wa Jimbo la Geita (Geita &
Sengerema). Maaskofu wa Shinyanga waliomtangulia ni Askofu Edward Aloysius
McGurkin aliyekuwa Askofu wa Shinyanga kati ya tarehe 04 Julai 1956 hadi
alipostaafu 30 Januari 1975.
Pia alitanguliwa katika kiti cha uaskofu wa Shinyanga
na Askofu Castor Sekwa aliyekuwa Askofu wa Shinyanga kati ya tarehe 08 Agosti
1975 hadi O4 Juni 1996. Askofu McGurkin, ambaye alikuwa raia wa Marekani
alifariki tarehe 28 Agosti 1983 na Askofu Sekwa alifariki tarehe 04 Juni 1996.
Kuna hadithi ambayo
sikuwai kuidhibitisha; lakini inasemekana Askofu Balina alibatizwa kwa jina la
‘Aloysius’ baada ya wazazi wake kuchagua jina hilo
ili afuate mifano mizuri ya kumcha mungu kama
alivyofanya Padri Edward Aloysius McGurkin mbaye alikuwa Paroko wao. Na jambo
hili kweli lilitimia kwani ‘Aloysius mkubwa’ na ‘Aloysius mdogo’ wote waliweza
kuwa maaskofu kama nilivyoelezea hapo awali.
Askofu Balina alikuwa
akisumbuliwa na
maradhi ya saratani ya ini kwa muda mrefu. Alikwishatibiwa Ujerumani na Vaticani, na akarejea nchini akiwa mwenye afya njema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...