Mzee Aidan Hassan Libenanga enzi za uhai wake.
 Mkuu wa wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro Anthony Mtaka akitoa salamu za uongozi wa mkuu wa mkoa huo Joel Bendera wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Aidan Libenanga nyumbani kwake.
 Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood akitoa heshima za mwisho kwa mwandishi Aidan Libenanga wakati wa kuaga mwili huo nyumbani kwake kota za Sabasaba Kiwanja cha Ndege shughuli iliyoanza majira ya saa 7 mchana.
 Meya wa Manispaa ya Morogoro Amiri Nondo naye akitoa heshima hizo.
Mratibu wa miradi wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro (MOROPC) Thadei Hafigwa akiaga mwili wa marehemu Aidan Libenanga muda mfupi kabla ya kuelekea katika makaburi ya Kola kwa ajili ya mazishi ya mpendwa wetu. 
 Ramadhan Libenanga na kaka yake aliyembeba mtoto wakiaga mwili wa baba yao.
 Mwandishi wa IPP MEDIA mkoa wa Morogoro Devotha Minja naye akitoa heshima zake za mwisho.
 
 Mtoto wa marehemu Aidan Libenanga, Ramadhan Libenanga wa kwanza kushoto akishirikiana na ndugu, jamaa na marafiki wakiingiza jeneza katika kaburi wakati wa mazishi ya mwandishi huyo wa habari aliyefariki dunia Nov 18 mwaka huu mkoani Morogoro.
 Mke wa marehemu, Aidan Libenanga, Elizaberth Libenanga (katikati) akisindikizwa na rafiki zake kuweka shada la maua katika kaburi la mume wake katika makaburi ya Kola.
 Waandishi wa habari mkoa wa Morogoro na mikoa ya jirani wakiwa na mishumaa wakiwasha kwa ajili ya kuweka katika kaburi la mpendwa wao Mzee Aidan Libenanga baada ya shughuli za mazishi kukamilika.
 Ndugu wa karibu wa Mzee Aidan Libenanga wakiangua kilio mara baada ya kuaga mwili wa mpendwa wao.
Ni huzuni na vilio kwa ndugu, jamaa na marafiki wakati wa kuaga mwili wa Mzee Libenanga.
 Mmoja wa watoto wa Mzee Libenanga akiwa ameshikwa na ndugu kuelekea katika gari kwa ajili ya kwenda makaburini.Picha Zote na MdauJuma Mtanda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Haya majina ya kibongo yanachanganya, Hassan na msaraba haviendani. Mwe!!

    ReplyDelete
  2. JINA SIYO DINI. ULISHAWAHI MSIKIA DR. THOMAS KASHILILA AU EDWARD MHINA NA DINI ZAO?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...