Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa  Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,pamoja na Viongozi wengine wa Vyama na Serikali,katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo,akielekea Nchini Vietnam kwa ziara rasmi ya Kiserikali,katika ziara hiyo Rais amefuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na Mawaziri na Maofisa mbali mbali 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,pamoja na Viongozi wengine wa Vyama na Serikali,katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo,akielekea Nchini Vietnam kwa ziara rasmi ya Kiserikali,

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakiagana na wazee wa chama na Maofisa mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiagana na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi,katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar,akielekea Nchini Vietnam kwa ziara rasmi ya Kiserikali,katika ziara hiyo Rais amefuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,pamoja na Mawaziri na Maofisa mbali mbali.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

Na Rajab Mkasaba, 
Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein ameondoka nchini leo kuelekea nchini Vietnam kwa ziara ya Kiserikali kufuatia mualiko rasmi wa kiongozi wa nchi hiyo.

Katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, Dk. Shein aliagwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd pamoja na viongozi wengineo wa vyama na Serikali.

Katika safari hiyo ya wiki moja Dk. Shein amefuatana na mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na viongozi wengine wa Serikali akiwemo Waziri wa Kilimo na Maliasili Mhe. Suleiman Othman Nyanga, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdillah Jihad Hassan.

Viongozi wengine ni Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika Mhe. Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi Juma Maalim, Mshauri wa Rais, Ushirikiano wa Kimataifa na Uwekezaji Balozi Ramia Abdiwawa pamoja na Maafisa wengine wa Serikali. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Safari njema mkuu.Duh Vietman nakumbuka nilikvyokuwa mdogo kuna `picha` ya Missing in Action ya Chuck Norris(1984)raia wa vietnman wanavaa vikofia kama uyoga vile,wakibonyea chini ni balaa.Kwa Dar sinema enzi hizo zinatangazwa magazetini,Drive in,Avalon si ndiyo Ankal?

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...