Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.
Mwandaji wa mpambano wa ubingwa wa WBF Mohamed Bawazir katikati akiwa ameshika mkanda na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Fransic Miyayusho kulia wengine kulia ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa ambao na wasimamizi wa mpambano huo na Kushoto ni Mratibu Paul Kunanga na Kocha wa Nasibu Christopher Mzazi

======  =======  ====== ======

KAMPUNI YA Darworld Links imeandaa mpambano mwingine wa ubingwa wa masumbwi utakaowakutanisha bondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho, mpambano huo utakaofanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba,

Aakizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mohamed Bawazir,amesema  kuwa amewakutanisha mabondia hao kutaka kujua nani zaidi ya mwenzake kwa kuwa viwango vyao vina fanana na vinatambulika kimataifa hivyo amewataka watanzania kujitokeza kuwapa sapoti hususani kudhamini wa mchezo huo wa masumbwi.

Udhamini tunapoomba sehemu ya makampuni mbalimbali ukienda wanasema atuhusiki na mchezo huo,Wengine wanasema kabisa wadhamini wa michezo wakati wanabagua michezo mingine kama ngumi awapewi kipaumbele kabisaa

amewaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza siku ta 9 Desemba kuja kuangalia ngumi ili zisonge mbele watakaosindikiza mpambano huo wa masumbwi ni 
Fadhili Majia VS Juma Fundi Moh'd Rashid Matumla VS Doi Miyayusho
Ibrahimu Class 'King Class Mawe' VS Said Mundi wa Tanga
Fred Sayuni VS Deo Samweli Hassani Kidebe VS Baina Mazola

Mapambano yote ya utangulizi ni mazuri na vijana wanaotakiwa kuendelezwa katika elimu ya masumbwi Duniani ili wawe mabondia wazuri 

Mpambano huo umedhaminiwa na JB BELMONT HOTEL gazeti la Jmbo Leo, Times FM,Na wengine wameobwa kujitokeza katika udhamini huo kwa mawasiliano zaidi 
0716 332933
0784 426542.

KWA AJILI YA KUTOA SAPOTI YA AINA YOYOTE PAMOJA NA USHAULI KATIKA MPAMBANO HUU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Wajameni kwanini kuwavalisha over size coats?

    ReplyDelete
  2. Aisee Uncle ni nani kawevesha hawa bwana (wanamasumbwi)hayo makoti aisee ?, ni kichekesho !

    ReplyDelete
  3. Ubingwa wa WBF ndiyo nini? uzito gani na/au mashindano gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...