Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi (kushoto) akiwaonyesha wawekezaji watarajiwa ramani ya eneo la Gwata, wilaya ya Kisarawe lenye ukubwa wa hekta 63,000 lililotengwa kwa ajili ya kilimo cha mpunga na miwa chini ya mpango maalum wa uendelezaji kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT). Baadhi ya maafisa wa serikali na SAGCOT waliwapeleka wawekezaji hao kama moja ya matukio ya mkutano uliomalizika hivi karibuni Dar es Salaam kuhusu uwekezaji katika sekta ya kilimo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi (kulia) akijadili jambo na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Chrostopher Chiza (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha mpango maalum wa uendelezaji kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Bw. Geoffrey Kirenga (katikati). Maafisa hao walikua pamoja na kundi la wawekezaji waliokwenda eneo la Gwata, wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani leo kuangalia eneo lililotengwa na serikali kwa ajili ya kilimo cha mpunga na miwa chini ya mpango wa SAGCOT.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Raymond Mbilinyi (kushoto) akijadili jambo na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Chrostopher Chiza (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha mpango maalum wa uendelezaji kilimo katika ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Bw. Geoffrey Kirenga ndani ya treni ya Tazara leo jijini Dar es Salaam. Maafisa hao walikua pamoja na kundi la wawekezaji waliokwenda eneo la Gwata, wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani kuangalia eneo lililotengwa na serikali kwa ajili ya kilimo cha mpunga na miwa chini ya mpango wa SAGCOT.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...