Kwako Ankal na wadau wa blog hii bomba...
Nna kitu ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikinisumbua, na leo baada ya kusoma malalamiko ya wachezaji wa Simba wazalendo kufanya mgomo baridi kwa msalahi duni wakati wenzao wa kutoka nje wakila bata mbele yao imenilazimu nitie neno leo.
Sitaki kuongelea mambo ya simba wala kilabu kingine chochote bali ni hii dhana nzima ya wachezaji kulipwa mishahara, tena hadharani na kwa mikataba. Ina maana Tanzania sasa ina michezo ya kulipwa?
Nauliza hivyo kwa sababu kama sikosei Katiba ya nchi inaweka wazi kwamba katika Tanzania michezo ni ya ridhaa. Kwa hiyo kama wanasoka Tanzania wanalipwa mishahara ina maana soka sio tena mchezo wa ridhaa. Je, hapo TFF na vilabu havivunji Katiba ya nchi?
Kwa mchezo wa ndondi kuwa wa kulipwa naona ni sawa maana hata usajili wake unafanywa na msajili wa makampuni, na sio Wizara ya Vijana, Habari Utamaduni na Michezo, ambako kupitia kurugenzi ya michezo, ndio wasajili wa taasisi kama TFF na vyama vingine vya michezo ya ridhaa. (Naomba kusahihishwa kama nimechemka). Hivyo basi naomba kujua ni lini soka limeidhinishwa kuwa ni mchezo wa kulipwa (profeshno)?? Je kinachoendelea sasa kiholela hapa nchini si uvunjifu wa Katiba?
Najua nitashambuliwa na waliozoea kuzoza bila kufikiria kwanza, lakini siogopi maana msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Natoa changamoto kwa serikali, hususan Wizara inayoshughulikia michezo iliangalie swala hili kwa mapana yake, sio kwenda mpururo tu tena kwa mazoea kama ilivyo kibongo-bongo...Tulinde na kuheshimu katika Jamani....
Nawasilisha
Mdau Dodoma
Kaka ulioeleza nakuunga mkono sana kwa yote uliyozungumza,tatizo la nchi yetu inachozungumza yaani SHERIA haiyeleweki kila kazi ni kazi ikiwa ubunge au kucheza mpira,KUCHEZA NGOMA pia ni kazi kwa hiyo kwanza kabisa walekebishe hizo katiba zao au sheria zao zinazo sema mpira au michezo ni RIDHAA,wao kutukana majukwaani ndio kazi au ushoga?au ndio SIASA?inavyosema watukanane kama watoto wa mitaani wasiokuwa na wazee?asante mdau kwa mada yako tunataka wachezaji wetu walipwe vizuri SOKA la ndani ikiwa kunaonekana maendeleo SOKA BILA YA PESA haiwezekani WATANZANIA
ReplyDeleteTunaomba majibu kutoka kwa wahusika.Asante mdau wa Dodoma.Vipi hapo mambo ya Maisha club Dodoma?
ReplyDeleteDavid V
ILI KUTOA NAFASI YA SOKA LA TANZANIA KUPANDA NA KUWA LA KULIPWA, INATAKIWA KUJITOA MUHANGA KWA MAMBO MATATU (3) HAYA HAPA CHINI:
ReplyDelete1.KUZIUA KLABU MBILI ZA MPIRA AMBAZO ZIMEKUWA KAMA 'HIRIZI' ZA UCHAWI ZINAZODUMAZA MAENDELEO YA SOKA NCHINI. (i)Yanga SC, (ii) Simba SC
2.SHERIA ZA UENDESHAJI WA VILABU VYA MICHEZO ZIWE ZA KIBIASHARA NA KUWA SOKA ISICHUKULIWE KAMA BURUDANI.
3.'UTU UZIMA DAWA'
WAZEE NI MUHIMU KTK MAISHA YETU NA MCHANGO WAO NI MKUBWA KTK MUSTAKABALI WETU, ISIPOKUWA WAZEE WABAKI KAMA WASHAURI WATAFUTWE KWA USHAURI NA SIO KU INFLUENCE MAAMUZI NA UENDESHAJI WA VILABU.