Reserve Bank of India (RBI) imeiandikia serikalli ya nchi hiyo kuitaka ijipange upya  au irekibishe baadhi ya sheria ili benki inayofuata sheria za kiislam iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi. 


Akizungumzo hayo governor wa benki hiyo Bw. D, Subbarao amesema ‘benki zinazofuata sharia za kiIslam zimeruhusiwa ktk nchi nyingi duniani, lakin sharia za India hazifanani na zile zinazofuata sheria ya kiIslam kwasababu benki hizo zinakopeshwa kwa riba wakati zinapokopa kutoka kwa RBI. Ispokua tuko ktk mazungumzo na serikali ili iweze kuruhsu benki hizo kufanya kazi zake kwa ufanisi nchini India’.

Itakumbukwa kwamba serikali ya Uingereza ilibalisha sheria ya kodi mwaka 2003 ili iweze kuziruhusu bemki za kiIslam kufanya kazi zake kwa ufanisi. Mpaka mwaka 2003 Mortgage inayofuata sheria za kiIslam kilikua ni kitu hakifahamiki vizuri nchini uingereza, kwa sababu ilikua ikitozwa kodi mara mbili na kuifanya iwe ghali zaidi kuliko mortgage za benki zisizokua za kiIslam. Kwa mfano, hilo linatokea wakati banki inaponunua nyumba kwa malengo ya kumuuzia mteja. Benki inatoa kodi wakati inaponunua jingo kutoka either kwa benki nyingine au kwa mteja na kodi hiyo inatolewa tena wakati benki itapoiuza nyumba hiyo kwa mteja kwa kutumia kitu kinachojulikana kama (Murabaha). Biashara hiyo ni lazima ifanyike mara mbili kama biashara tofauti ili iweze kua halali kwa sharia za kiIslam.

Baada ya kufahamishwa the Chancellor of the Exchequer kuhusu swala la benki hizo kutoa kodi hiyo marambili, sheria ilibadilishwa kwa benki za kiIslam na zikaruhusiwa kutoa kodi hiyo mara moja tu. Tangu kubadilishwa kwa sheria hiyo benki kubwa kama vile HSBC na the Lloyds TSB walianza kutoa mortgage zinazofuata sheria za kiIslam. Kwa maelezo zaidi wasiliana na http://ijuebankyakiislam.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. KANUNI YA KIFEDHA YA KIISLAMU YA KWA KIWANGO CHA RIBA KUWA 0% HAINA MPIANZANI KTK BENKI KUU ZOTE DUNIANI.

    MSILETE UBISHI HADI MASHIRIKISHO YOTE YA KIDUNIA KAMA UN, IMF, WORLD BANK NA DEVELEOPMENT PARTNERS WOTE WANAIKUBALI!!!

    SASA IWEJE WEWE ''SAMSONI DELILA'' WA TANZANIA UNAIKATAA, NAKUDAI NI KULETA UDINI???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...