Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhili Soraga ambaye amelazwa katika chumba cha dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia majeraha ya usoni na kifuani yaliyotokana na kurushiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe mjini Unguja juzi. Rais ambaye amerejea jana Jumanne, akitokea katika ziara ya kikazi ya takriban juma moja katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida, amemtakia Sheikh Soraga nafuu ya haraka. (PICHA NA IKULU)
JESHI LA POLISI ZANZIBAR LAANZA UCHUNGUZI WA TUKIO LA KUMDHULU KATIBU WA MUFTI ZANZIBAR
Na Mohammed Mhina,
wa Jeshi la Polisi-Zanzibar
JUMANNE NOVEMBA 6, 2012. Jeshi la Polisi Zanzibar, limeanza uchunguzi na msako wa kuwatafuta wale wote waliohusika kwenye tukio la kumwagia maji makali Katibu wa Mufti wa Zanzibar Sheikhe Fadhil Soraga, alfajiri ya leo (Novemba 6, 2012) wakati akiwa mazoezini mjini Zanzibar.
Taarifa ya Afisa Habari Mkuu wa Jeshi hilo Visiwani Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, imesema kuwa Jeshi la Polisi Visiwani humo limeanza uchunguzi na msako mkali wa kuwabaini na kuwatia mabaroni wale wote waliohusika katika shambulio la Katibu huyo wa Mufti Zanzibar.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari kwa nyakati tofauti leo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar ACP Yusufu Ilembo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, ACP Aziz Juma Mohammed, wamesema kuwa Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Kamanda Ilembo amesema Jeshi la Polisi limesikitishwa na kitendo alichofanyiwa Sheikhe Soraga na kwamba wanakichukulia kama kitendo cha kihalifu.
Kamanda Ilembo amesema Jeshi la Polisi litahakikisha kuwa wale wote waliohusika na tukio hilo, wanabainika, kukamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili na hatimaye sheria kuchukua mkondo wake.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa tayari ameunda kikosi kazi cha Makachero watakaokusanya taarifa za kubaini njama na watekelezaji wa tukio hilo la kumwagia sheikhe huyo maji hayo yenye ukali.
Amesema Shekhe Soraga, alimwagiwa maji hayo katika viwanja vya Mabata vilivyopo karibu na Msikiti wa Msumbiji akitokea upande wa Uwanja wa Michezo wa Aman kwenda Mwanakwerekwe ambapo akiwa katika eneo hilo alikutana na mtu mmoja ambaye naye alionekana kama mchukua mazoezi akitokea upande wa Mwanakwerekwe kuelekea Uwanja wa Aman na walipokuwa wakipishana ndipo alipomwagiwa machoni maji hayo yenye ukali.
Amesema baada ya tukio hilo Sheikhe Soraga alikaa chini kwa maumivu na baada ya kuda kidogo alipata wasamalia wema na kumchukua hadi kwenye Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ambako alipatiwa matibabu ya awali kabla ya kusafirishwa kwa ndege ya Serikali kwenda Dar es Salaam ambako amelazwa katika Hospitali ya Agha Khan kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Naye Mufti wa Zanzibar Sheikhe Salehe Kabi, amewataka Wananchi wa Zanzibar kuacha visa vya kulipiziana visasi vitendo ambavyo vinaweza kuleta vurugu na kuzua mtafaruku katika nchi yetu.
Aidha amewataka watu wote kuwa wamoja na kushirikiana kwa kila jambo na kwamba tofauti za rangi, kabila, dini na itikadi za kisiasa ziwe chanzo cha mafarakano ya Umoja wetu.
Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, Sheikhe Soranga, alisindikizwa na Makamu wa Pili wa Rais balozi Seif Ali Iddi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mh. Abdallah Mwinyi na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama na Mashekhe.
Wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa kujua aina ya maji hayo pamoja na kuwapata waliohusika katika tukio hilo, Jeshi hilo limewataka wananchi kuwa watulivu na kutoa ushirikiano wa kuwabaini wale wote waliohusika katika tukio hilo.
Jeshi la Polisi Zanzibar ni sawa na gari bovu maana kila siku liko geraji kutengezwa. Kesi zote za kisiasa zilizotokea Zanzibar hajawahi kupatika na hatia hata mtu mmoja.
ReplyDeleteJAMANI HUU SI UUNGWANA KABISA KWA ALIYEFANYA TENDO HILI. POLE KATIBU MUFTI
ReplyDeleteMbona shuka hapo kitandani linaonekana kama jipya kabisa, au ndio maandalizi kwa kujua mheshimiwa anakuja kumuona mgonjwa!?
ReplyDeleteNadhani ni vema kuacha mh. aone mambo halisi yalivyo (bila shaka anajua tayari hata hivyo)
Kwa nini kafanyiwa hivyo tuelezeni kisa.na Kwa nini viongozi wa serikali wawe pamoja nae hivi? mhhhhh kuna kitu. tuwelezeni. siwezi kusema kitu mpaka nijue mkasa kamili
ReplyDeleteDuh, Rais amerespond haraka sana, ni kama ilikua kwenye ratiba zake
ReplyDeletePole sana Katibu...
ReplyDeletelakini tunataka kujua nini chanzo??
mbona kama yale ya Arusha??
huu ni upuuzi tu wa watu wachache wanaotaka kuchafua hali ya amani...Tunakuomba tena Dr Shein hawa watu wanaendelea kuharibu hali ya hewa.Inafika kikomo na sie tutasema basi liwalo na liwe. Tunakusisitiza tena upole wako utawaponza na wengine.Tumechoka na sie tutalipiza.
ReplyDelete