Rais Jakaya Kikwete akiangalia chupa ya tangawizi iliyotayari kuuzwa mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda cha kuzalisha Tangawizi kimnachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mambakatika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.
Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kinachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda wakati amkaribisha kufungua kiwanda cha kusindika Tangawizi.
 Rais Jakaya Kikwete akifungua rasmi kiwanda cha kusindika tangawizi katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Kushoto ni Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kimnachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda  na Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho kwa asilimia kubwa.
 Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda hicho katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Kushoto ni Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kimnachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda
 Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kufungua rasmi langop kuu la Kiwanda hicho.
 Rais Jakaya Kikwete akikagua uzalishaji wa Tangawizi mara baada kufungua rasmi kiwanda cha kusindika Tangawizi kinacho milikiwa na Ushirika wa wakulima wa Tangawaizi katika Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.
 Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kinachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda (kushoto) juu ya shughuli za uzalishaji mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda hicho katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho kwa asilimia kubwa.
 Rais Jakaya Kikwete akioneshwa chupa ya tangawizi iliyotayari kuuzwa .Kushoto  ni Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kinachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda akimpa maelezo  juu ya shughuli za uzalishaji mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda hicho katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.
 Rais Kikwete akisalimina na wananchi wa rika mbalimbali waliofurika katika uiwanja wa michezo wa Goha kata ya Mamba Miamba kumsikiliza.
 Rais Jakaya  Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha shukrani Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela kwa kufanikisha ujenzi wa Kiwanda cha kusindika tangawizi katika Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro. Rais Kikwete alifungua kiwanda hicho juzi.
 Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Mhe. Anne Kilango Malecela akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kabla ya Rais Kikwete kuhutubia hadhara hiyo.
Rais Jakaya  Mrisho Kikwete akiwahutubia wakazi wa Kata ya mamba Miamba wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Picha na Father Kidevu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hakika Mhe Anne Kilango ni wa kupewa tuzo la kipekee jinsi alivyojituma kwa watu wake wa Jimbo la Same Mashariki. Ni vyema jirani wa Same Magharibi akaiga maendeleo hayo sio kukaa na vyeo ambavyo havisaidii wananchi. Same Mashariki Oyeeee. Ernest Mnzava

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Anna Kilango. Jamani, just imagine, endapo kila mbunge angebuni mradi mmoja tu katika jimbo lake, Tanzania ingekuwa wapi hivi sasa? Kabla ya uzinduzi huu, hiyo tangawizi ilikuwa inaharibika tu na wakulima hawapati faida yoyote ile ya jasho lao. Hakika, huyu mama Mheshimiwa atapata thawabu nyingi sana kwa kuwakomboa hao wapare wenzake kutoka kwenye lindi la umaskini. Hongera sana sana dada Anna, kweli umethibitisha nia yako ya kuwaondolea watanzania umaskini........

    ReplyDelete
  3. HONGERA SANA MAMA KILANGO,UMEONYESHA MFANO KWA VITENDO,MUNGU AKUSIMAMIE KWA KILA JAMBO.

    ReplyDelete
  4. KASI HII YA UTEKELEZAJI WA SERA ZA CCM YAFAA ITANDAE KWA KUWAWEZESHA VIJANA NCHINI KOTE ILI WAWE WAJASIRIAMALI.

    TAASISI ZA FEDHA ITIKIENI WITO HUU BILA KUJIMINYA, KWANI MAZINGIRA HAYA YAMEANDALIWA NANYI YABORESHENI KWA VIJANA BILA UBAGUZI.

    MAINA OWINO
    UK

    ReplyDelete
  5. Mh. Anna pongezi sana sio tu kwa usimamiaji na kutafuta fedha na mikakati bali kwa ubunifu na kuweka mguu chini bila kuyumbishwa. sisi wananchi tunajua nani kiongozi wa kweli. itafika wakati rushwa itashindwa....hongera mama na wamama woote wenye jitihada kama za Anna.

    ReplyDelete
  6. MIMI NDIMI NJIA NA KWELI NA UZIMA!..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...