Kaka Michuzi kwanza nikushukuru kwa ajili ya kuweka kwenye blog yako tukio kabla na baada ya Campus Night Event.
Pili nikuombe unisaidie kuweka tukio ambalo limenitokea jana tu.
Amini usiamini-uhuni unaofanywa na DUWASA
Ni tukio la kweli limenitokea mimi mwenyewe na watu wengine wengi wameathirika na huu uhuni wa watoa huduma hii.
Mwezi uliopita msoma mita ya maji hakufika kusoma mita na hivyo akakadiria matumizi yangu ya maji kufikia karibu 60,000/= kwa mwezi mmoja tu ilihali matumizi yangu kwa wastani hayazidi 25,000/= kwa mwezi.
Kama mteja mzuri nikaenda kuhojiana na maofisa wa DUWASA wakasisitiza na kuonya kwamba lazima nilipe hio ndio taarifa ya msomaji na msomaji akathibitisha kwamba alisoma. Nikahamaki kuwa alisoma mita gani, alipitia mlango upi ambao watu waliopo nyumbani kwangu hawakumfungulia wala kumuona.
Kukatisha hayo nikaamua kulipa 35,000/= ilihali baadae nimalizie deni lao.Hii ilikuwa ni kama wiki mbili zilizopita.
Nikiwa safarini kurudi nyumbani, nikapigiwa simu na kiongozi wa operesheni kata maji wa DUWASA kuwa wanakata maji nyumbani kwangu. Nikawasihi kwamba nitailipa nikifika tu, hawakutaka kunisikia na wakaendelea na zoezi.
Nikawauliza kulikoni kukata maji? Wakasema nadaiwa Tsh 53,000/= na kwamba tofauti ya fedha ya ile niliyoacha kulipa mweizi uliopita inaongezwa na bili ya mwezi huu. Cha ajabu, bili hio inayosemwa ya mwezi huu, haijawahi kuletwa kwangu (Iko kwenye komputa zao za ofisi).
Nilipoenda kulipa nirudishiwe maji nilitakiwa kulipa pamoja na bili yangu, 20,000/= ya penati ya kukatiwa maji. Nimekuwa mteja wao mzuri na sijawahi kuvusha kulipa bili hata ya mwezi mmoja kuacha hii yenye matatizo.
Cha ajabu zaidi ni kwamba nilipata habari zingine toka ndani ya shirika kwamba hali ni mbaya ya kifedha kwa hiyo wamebuni mbinu ya kuongeza mapato. Watu wengi wamekatiwa maji kwa mtindo huu. Najiuliza maswali haya: Hivi ndivyo unavyohusiana na mteja wako? Hii ni njia sahihi ya kupata fedha kwa watu unaowategemea kulipa mishahara yako?
Haya yataendelea hadi lini?Kuna mtu ana haki ya kuchezea haki ya msingi ya maji kwa sababu ya mahitaji yake binafsi? Huu ndio uungwana kwa watanzania wenye matatizo lukuki? Ni sawa kumlazimisha mtu kuacha kufanya kazi zenye kuongeza kipato akashughulikie kurudisha maji nyumbani kwake?
Naomba wahusika washughulikie huu unyanyasaji wa karne ya sita wala si hii ya 21.
Naomba kuwasilisha
Ibra


Kusema kweli hawa ndio zao kubambukiza watu bili za maji.
ReplyDeleteMimi niliwekewa maji na nililipa gharama zote na mwezi huo nilipata maji mara 3 kwa mwezi na bili waliyoileta ni shs 185,000/=! nilienda kulalalamika wakaibadilisha na kuwa 40,000/=! kwa unyonge niliamua kulipa.
Mwezi uliofuata sikupata maji kabisa lkn waliniletea bili ya shs 85,000/= pamoja na kuwa mita ipo!
Nilienda kulalamika na niliwaambia waje wang'oe UCHAFU wao sitaki tena maji yao nitanunua na kuweka ktk kisima INATOSHA!
MIe kama ningekutana na mhusika huyu home kwangu wallah ningeweza 'kumchoropoa' utumbo kwa hasira
my dear Ibra pole sana kweli nakunga mkono kwa hawa watu wa DUWASA ni washenzi sana haswa hao watu wanaozunguka na magari wanakula rushwa ile mbaya. Utakuta asubuhi wameishafika nyumbani kwako kabla hujatoka na ukiongea nao wanataka kitu kidogo(pesa) na ukiwapa basi hawatakata wataondoka na kukwambia uwende lipa.
ReplyDeleteWatachukuwa na simu yako kwa kuwa wamekuwa rafiki zako, basi mwezi unaofuata wakileta bill tuu hao wameishafika au kukupigia simu tunakata maji ukiwambia subiri wanasema tutarudi badaye jamani na kweli wanakuja kama vile deni lazima uwape kitu kidogo kwa vile wameisha zoea.
Mimi niliamua wakate maji kwangu huo usumbufu sina tena na njia zangu natumia kupata maji bila tabu.
WAZIRI WA MAJI PLEASE TUNAOMBA UWASHIKISHE ADHABU WATENDAJI WAKO WA KAZI WANAKUTIA AIBU. WEWE UNA RAHA ZOTE WANANCHI WAKO WANATABIKA KWELI HII HI HAKI CHUNGUZA UTAONA AIBU KWA HILO. UKO JUU HUYAONI HAYA RUSHWA TUPU IMEJA KWENYE WIZARA YAKO KISIRI SIRI. IT'S TIME TO TAKE ACTION SIO BLAA BLAA!
Mdau
Tahadhari hakikisha unachokiongea kiwe a ukweli kwa sababu hilo ni shirika la umma na lina waasheria wake, usije ukajikuta unahojiwa na kuishia uashindwa kuthibitisha
ReplyDeletetatizo letu watanzania tunapenda kulalamika na hatutimizi wajibu wetu.kama mita haijasomwa,unafanyaje?ulitoa tarifa DUWASA baada ya mita kutokusomwa?wewe ndo wa karne ya sita.cause huwajibiki unaishia kulalamika,tena kwa makosa yako. mi naona DUWASA wanajitahidi ukilinganisha na eneo lenyewe(UKAME).wewe utakuwa ni mgeni dodoma.wenzako tunaborekaga lakini tukikumbuka wakati wa DOWICO,Matoroli na madumu ya maji tunatulia.timiza wajibu wako kaka acha kulalamika na kupotosha.
ReplyDeleteHiyo ni kweli kabisa. Hata mimi nilishabambikizwa deni wakijifanya walisoma mita. Mashirika haya yanahitaji wapinzani ili kufanya kazi kwa ufanisi
ReplyDeleteni kweli hawa DUWASA wa dodoma wamezidi. leo nimewasikia wanapita barabarani wakitangaza kwamba wanaanza operesheni kata maji. sio haki kabisa kumkatia mteja maji kwa deni la mwezi mmoja tu, hata kama wameishiwa hela sio kiivyo sasa, tutang'oa maji yao tuchimbe visima tu.
ReplyDeletebili zao kwanza ni za kukisia tu kimakadirio, haiwezekani mwezi mmoja ulipe elfu 20, matumizi yako ya kawaida tu lakini mwezi unaofuata utakuta bili inakuja elfu 70
Sasa kutokulipa mwezi mmoja na maji yametumika, unadhani gharama zilizotumika kutoa maji Mzakwe takribani kilometer 40 anazilipa nani? kama sio wewe mwananchi (ni haki kukata maji kwa mwezi mmoja)na kuchimba kisima huzuiwi ila omba kibali maana utalipishwa kisawasawa iwapo hutaomba kibali, ukiona bili ni ya kukisia, hawa jamaa DUWASA wana 'Customer Service' na pia wana namba za simu za bure kwanini usiwaendee hewani? Kwa taarifa yako wapo watu wanatumia maji zaidi hata ya 300,0000 na ni matumizi ya kawaida tuu. Hata siku moja usihukumu shirika maana hata kama anayetenda kosa ni mmoja basi si shirika nzima mfano TANESCO mtu mmoja tu ndiye anayekuja kusoma meter yako na si shirika lote, waendee ili wajue kosa limeanzia wapi maana ni msomamita mmoja ndiye aliyekuja kusoma meter yako. Mteja wa Duwasa
ReplyDelete