Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dkt. Idris Rashidi akizungumza na waadishi wa habari (hawapo pichani) katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa kuanzishwa Amana Bank na wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Afisa wa Benki hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dkt. Idris Rashidi akihudumia Mteja katika Tawi la Tandamti- Kariakoo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja.
Amana Bank wiki hii inaadhimisha kutimiza mwaka mmoja tangu ilipofungua milango kwa wateja mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2011. Maadhimisho haya yanaambatana na wiki ya Huduma kwa Wateja ambapo Amana Bank inatoa nafasi kwa wananchi na wateja kujifunza zaidi juu ya huduma zake.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dr. Idris Rashidi alisema, “Tumeamua kusherekea mwaka mmoja wa Amana Bank kwa kuanza na wiki ya huduma kwa wateja. Wiki hii ilianza tarehe 19 Novemba na itakamilika tarehe 23 Novemba 2012. Lengo la kuweka wiki hii ni kuwapa fursa wateja wetu na jamii kwa ujumla elimu kuhusu huduma za kibenki zinazofuata Sharia kikamilifu”.
Amana Bank inajivunia kuwa benki ya Kwanza Tanzania inayofuata Sharia kikamilifu ikiwa na lengo la kutoa huduma za kibenki za kisasa na za kipekee zinazofuata Sharia kwa kuzingatia maadili na kwa njia iliyowazi kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wadau wote.
Katika kipindi ha mwaka mmoja Amana Bank imefanikiwa kufungua matawi matatu ambayo ni Tawi la Tandamti lililoko mkabala na soko kuu la kariakoo, Tawi la Barabara ya NYERERE BRANCH na Main Branch.
Pamoja na mtandao huo wa matawi Amana Bank pia imeongeza huduma ambazo zinalenga kumrahishia mteja kupata huduma za kibenki popote alipo. Hivi karibuni benki ilizindua huduma ya Amana Mobile Banking. Huduma hii inamuwezesha mteja kupata huduma kupitia simu yake ya mkononi. Kupitia huduma hii mteja anaweza kujua salio la akaunti yake, kununua muda wa maongezi, kuomba kitabu cha hundi n.k. Amana Internet Banking ni huduma nyingine ambayo imezinduliwa na Amana Bank. Huduma hii inamuwezesha mteja kupata huduma za kibenki kupitia mtandao wa intaneti.
Vilevile Amana Bank imeongeza huduma za kulipia kodi za Mamlaka ya Mapato (TRA) na ushuru wa forodha kupitia matawi yetu. Mteja wa Amana Bank na hata wasio wateja wanaweza kulipia kodi kupitia matawi yetu.
Amana Bank pia imerahisisha utumaji wa fedha popote pale duniani kwa kutumia huduma ya Western Union. Western Union ni huduma iliyosambaa duniani kote hivyo hurahisisha utumaji wa fedha za wateja na hata wasio wateja.
Dr. Idris Rashidi alisema, “Amana bank imepiga hatua kubwa katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho imekuwa ikitoa huduma za kibenki. Changamoto kubwa benki inayokutana nayo ni ufahamu mdogo wa wateja na jamii kwa ujumla juu ya huduma za kibenki zinazofuata Sharia. Benki inajitahidi sana kutoa elimu kwa umma kupitia wafanyakazi wetu ambao wamepewa na wanaendelea kupewa mafunzo juu ya huduma zetu”.


safi sana,tunaiman kuna mafanikio makubwa yanakuja kwa amana bank.
ReplyDelete