POLISI mkoani Morogoro imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi mil 7.6 baada ya kukamata makosa 267 ya usalama barabarani katika kipindi cha siku mbili.
Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi mkoani humo Faustine Shilogile amesema makosa hayo yalikamatwa novemba 24 na novemba 25 mwaka huu.
Kamanda Shilogile amesema makosa ya usalama barabarani yaliyokamatwa novemba 24 ni makosa 146 ambapo makosa 141 yamelipishwa faini na kukusanywa jumla ya shilingi mil 4,230,000.
Amesema hakuna mtuhumiwa aliyepewa onyo kutokana na makosa hayo ambapo hakuna watuhumiwa waliofikishwa mahakamani.
Aidha makosa 121 ya usalama barabarani yalikamatwa novemba 25 mwaka huu ambapo makosa 115 yamelipiwa faini na kufanya makusanyo ya shilingi mil 3,450,000.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Leonard Richard Gyndo amesema makosa hayo yamekamatwa kufuatia utaratibu wa kukusanya makosa ya kila siku yanayotokea ya usalama barabarani.
Kamanda Gyndo ameyataja baadhi ya makosa hayo kuwa ni makosa ya mwendo kasi , ubovu wa magari, kutofuata ratiba, kuzidisha abiria na matumizi mabovu ya barabara hasa katika eneo la nanenane kituo cha mafuta cha Oil com .
Pia amesema madereva wamekuwa na tabia ya kupitana kwa mbele (overtake) bila kuangalia eneo hilo ambalo lina michoro isiyoruhusu kupita na kujaribu kusababisha ajali.
Hivyo amewataka madereva kuwa makini wakati wanaendesha magari na kuhakikisha wanafuata alama za barabarani ili kuepusha ajali ambazo zinaeoukika.


.jpg)
Hesabu hii sio sawa. Kuna nyingine zilizoishia mifukoni hatujapewa hesabu yake. Au ndio tuendelee kujifanya kama vile tatizo la rushwa halipo? Wakati umefika wa kupiga vita suala hili katika kila eneo hapa nchini. Ikiwa serikali inashindwa kutulinda katika tabia hii sugu, inabidi sisi wananchi wenyewe tutafute mbinu za kujilinda ili taifa lisije likaangamia.
ReplyDeleteTatizo hapa sioufatiaji sheria watatu wasipofata sheria wewe ukifata utajikuta unagongana na wasiofata sheria na utaambiwa wewe ndio unakosa.
ReplyDeleteNa zilizo ingia mifukoni ni ngapi?
ReplyDeleteHahaaaa watuambie zingine zimeenda wapi? Mimi tu nimelipa zaidi ya laki 2. Inamaana tupo thelasini 30. Tuliolipa faini . Ha haaa haiingii kichwani kabisaaa. Hebu watuambie dala dala ngapi dar zilikamatwa ..ha haaaaaa. Kweli wajinga ndio wadanganywao...
ReplyDeleteUandishi mwingine bwana, 'makosa 115 yamelipiwa faini na kufanya makusanyo ya shilingi mil 3,450,000'. Sasa hii ni shs bilioni ngapi sijui.
ReplyDeleteMwandishi wa taarifa hii unatakiwa ujifunze namna ya kuandika hizo pesa, umesema jumla milioni 7.4, lakini baadaye unaongelea mil 3,450,000 hukutakiwa kuweka neno milioni hapo mbele, inachanganya msomaji
ReplyDeleteWajinga wao na hizo tarakimu zao. HATUDANGANYIKI...
ReplyDeleteMakosa watendao madereva barabarani kila siku ni mengi kupita kiasi.
Wenye kuendesha magari yenye tairi vibara,
Wasiovaa helmet,
wasiokua na leseni za udereva,
daladala zinazokatiza route,
daladala zinazopakia abiria mpaka wananingia mlanagoni,
daladala zinazopaki barabarani na sio kituoni ili kushusha na kupakia abiria.
daladala/magari yanayotanua kwenye foleni,
Wanaowafundisha watu kuendesha magari ya private wasiokua na leseni za class C na wala alama ya L mbele na nyuma ya gari na anaefundishwa hana provisional license.
Nitarudi baadae na makosa mengine kwa sasa najibrekisha.
hivi kumbe polisi inaweza kujitegemeaeeh!! maana hapo kama kungekua hakuna rushwa aka cha juu kwa polisi inamaana wangepata nyingi zaidi na wangejilipa wenyewe!!
ReplyDeletemilioni saba za serikali na milioni 270 zimeingia mifukoni
ReplyDeletemakosa ya barabarani ni mengi sana ukilinganisha na hesabu hiyo
tuendelee kuchakachua ipo siku tutalimana kwa majembe.
Dawa ya kuondoa rushwa ni kulipa faini. Tatizo ni wengine wanaona rushwa bora kulipa adhabu. Hivyo rushwa haindoki.
ReplyDelete