Taasisi ya Centre for Economic and Leadership Development usiku wa kuamkia leo imewatunukiwa baadhi ya viongozi wanawake barani Afrika akiwemo Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda kwa Mchango wao wa ushawishi katika maswala mbalimbali ya kuwainua wanawake barani Afrika. 

Hafla hiyo imefanyika jijini  Nairobi wakati wa mkutano wa mwaka wa taasisi hiyo uitwao "All Africa Women Leaders Summit and Award" ambapo Mke wa Waziri Mkuu wa Kenya Mhe. Dkt. Ida Odinga ndiye aliyekuwa Mgeni Rasmi. Mkutano huo ulifanyika kwa kauli mbiu iiitwayo " The role of Women leaders in reducing the vulnerability of the female adolescent and heads of households in Africa"
   Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akipokea tuzo iitwayo The African influential Amazon Award kutoka kwa Mke wa Waziri Mkuu wa Kenya Mama Dkt. Ida Odinga iliyotolewa na taasisi ya Centre for Economic and Leadership Development kutambua mchango wake katika kupigania maswala mbalimbali ya wanawake barani Afrika ikiwa ni pamoja na kushawishi wanawake kuingia katika vyombo mbalimbali vya maamuzi ikiwa ni pamoja na Bungeni., katika hafla iliyofanyika Mjini Nairobi Kenya
 Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja na Mke wa Waziri Mkuu wa Kenya Mama Dkt. Ida Odinga mara baada ya kutunukiwa tuzo hiyo huu mjini Nairobi.
Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...