Salaams Ankal,

Naomba waulize wadau kama wanaikumbuka hii taswira katika maisha

Mdau Umangani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Yeah iliniumiza kichwa sana enzi za udogo miaka ya mwanzoni mwa 80!!nilipata kujua jamaa alifikajefikaje katika mti ule.

    ReplyDelete
  2. Je, pana uwezekano binaadamu akaruka kama ndege?

    Kama itawezekana kuruka kama ndege, ndio suluhisho lililobakia hapo kama uwezekano huo hakuna, basi, hapo kilichobaki ni kumwachia Mwenyezi Mungu na Kusali kwa ISHARA !!!

    ReplyDelete
  3. Ya nini tabu?

    Imethibitika Kisayansi ya kuwa nyoka hana uwezo wa kung'ata wala kumeza akiwa juu ya mti.

    Hivyo nakabiliana na nyoka kwa kumjeruhi na kitu cha ncha kali kama vile ukucha wa kidole au kingine, mara akiwa na jeraha atanikimbia mimi sasa, hapo nakuwa Shujaa!

    ReplyDelete
  4. Mbona jibu ni rahisi sana hapo?

    Ni kugeuka kuwa YANGA halafu naruka chini na kukabiliana na kibonde wangu SIMBA!

    Kooote ni kugumu isipokuwa rahisi ni kwa Simba tu hapo.

    YAANI ANKALI PAMOJA NA KUIELEWA YANGA VIZURI NA WATU KIBAO WANA YANGA WAZURI MMESHINDWA KUPATA JIBU HILI?

    KWA VYOVYOTE NAJUA 100% NITAFANIKIWA KUCHOMOKA TU HAPO KUPITIA KWA 'MRAHISI WANGU' KIBONDE SIMBA!

    ReplyDelete
  5. Audhubillah
    Hii yaonekana kama ndoto mbaya, ni kama ile ya jinamizi.Sometimes life treats you like that, you feel surrounded, helpless and hapless, you have no way out. But there is always a way out, you need faith and trust.I think a little prayer and Divine intervention is required here?

    ReplyDelete
  6. PICHA HII INAJULIKANA KAMA "kisa cha mtema kuni"

    ReplyDelete
  7. KISA CHA MTEMA KUNI

    ReplyDelete
  8. Hapo njia ya Ukombozi ni moja tu!

    Nikuvuta pumzi nyingi halafu naruka hewani kama JET LI, napiga 'samasoti' za kinyume nyume za kuunganisha za juu kwa juu hewani, nawatoka wote hao kiulainiii !!!

    Wao kazi kwao ni vile wote hawana mbawa watakimbia kunisindikiza mwenzao nikiwa hewani!

    ReplyDelete
  9. hahahaha uncle hii picha ni ya zamani sana, nakumbuka zilikua zinauzwa sokoni kariakoo. kuna nyingine ya URAFIKI WA MASHAKA, simba anacheza na swala , nyoka na mbwa and the baaden vita.. hahaha

    ReplyDelete
  10. Mdau wa 4 hapo juu anony Wed Nov 28, 12:16:00 PM 2012

    -----------------------------------
    ITAMBUE AKILI YA ZIADA ILI KUOKOA MAISHA YAKO HAPO
    -----------------------------------

    MBINU HII NI KALI SANA, LAKINI INABIDI KWANZA UWE JASIRI NA SHUJAA.


    ...Kimbilio na matumaini ya mwisho ni kupitia MSIMBAZI KWA SIMBA!

    Nikujiachia kwa makini kutoka juu ya mti na kutua mgongoni mwa Simba lakini inabidi utue kwa stepu usije fikia mdomoni mwa mnyama yatakuwa mengine!, kama unavyomwona hapo chini anakusubiri kama mpira wa kona.

    Ukitua unatakiwa ufikie mgongoni mwake Simba halafu uyashike masikio yake huku na huku kwa mikono kama mpanda Farasi!

    Ukiwa mgongoni mwake kama mpanda Farasi utakuwa na uwezo wa kuyavuta masikio yake ili kumuamuru na kumuelekeza unakotaka kwenda na kwa mwendo kasi uutakao!!!

    Hapo utamtumia yeye mwenyewe Simba kukutoa katika eneo la hatari (ya hao wengine) kwa spidi ya moto chini mithili ya umeme!!!....shaaaaaaa!

    ReplyDelete
  11. Ohhh bosi hapo juu ya mti kazi anayo!

    ReplyDelete
  12. Mjomba Michuzi ungemjibu jamaa Mdau wa Umangani moja kwa moja ya kuwa Uchochoro wa kuponyoka hapo upo hapo kwa Simba tu.

    Ni kuwa jamaa angemwangukia simba kichwani kama furuhi la mzigo, mnyama wakati akiwa amepata maluwe luwe hajitambui jamaa angechukua nafasi hiyo kutoka mbio!

    Akaweza kujinusuru na hali hiyo tete iliyokuwa inamkabili akiwa juu ya mti!!!

    ReplyDelete
  13. Njia pekee za kujinusuru ni hizi:

    1.Jamaa kuwa jasiri na kumkaba nyoka kwa kabali ya miguu au mikono hadi nyoka anakufa.

    2.Jamaa kuwa jasiri kumshika nyoka halafu washuke wote hadi ndani ya maji halafu wakifika mamba watamgeukia nyoka na kuanza kupigana wakigombea kitoweo (mtu), wakati vita hiyo ikiendelea yeye jamaa atachukua nafasi hiyo kuogelea kuelekea ng'ambo ya pili ya maji upande usiokuwa na Simba.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...