SERIKALI inasikitika kutangaza kifo cha Bw. Jackson Makwetta kilichotokea Jumamosi saa 11 jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ya jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.
Msiba uko nyumbani kwake Boko kwa Wagogo. Taarifa zaidi kuhusu mipango ya mazishi zitatolewa baadaye.
Bw. Makweta aliwahi kuwa Waziri katika wizara mbalimbali zikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu kama Waziri wa Nchi, Elimu, Kilimo na Utumishi.
Pia amekuwa Mbunge kwa zaidi ya miaka 35.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA.
JUMAMOSI, NOVEMBA 17, 2012.
Mungu amlaze pema peponi na amsamehe kwa yote.
ReplyDeleteNakumbuka mwaka nilioanza kidato cha kwanza tambaza akiwa waziri wa elimu.