Mratibu wa Soka la Ufukweni a.k.a Beach Soccer,Shaffih Dauda akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kikao cha kwanza cha mkakati wa miaka minne ya maendeleo ya mchezo wa Soka la Ufukweni,ndani ya kiota cha cha Escape 2,Mbezi Beach jijini Dar,ambapo wadau mbalimbali wa Soka walishirikishwa na kutoa maoni yao ya nini kifanyike katika kipindi cha miaka minne ijayo walau Tanzania iweze kushiriki kombe la Dunia kupitia mchezo huu.
 Mkufunzi anayetambuliwa na FIFA wa mambo ya Utawala na uongozi michezoni,Henry Tandau (kushoto) akitoa somo kwa wadau waliohudhuria washa hiyo ya siku moja kwenye iliyofanyika kwenye kiota cha Escape Two,Mbezi Beach jijini Dar Es Salaam.
 Beki wa YANGA na nahodha wa zamani wa TAIFA STARS,Shadrack Nsajigwa akisikiliza kwa makini wakati wa semina ya kutengeneza mchakato wa maendeleo ya Soka la Ufukweli wa miaka minne, anayefuata ni winga wa zamani wa YANGA na RIVATEX ya nchini Kenya.
 Mratibu wa Soka la Ufukweni a.k.a Beach Soccer,Shaffih Dauda akiandika baadhi ya vigezo vinavyotakiwa kufuatwa wakati wa kuendesha soka hilo.
 wewe mdau pia unaweza kuongezea madini hapa!
 Ibrahim Masoud 'Maestro' alikuepo pia,pembeni yake ni Stewart Kambona kutoka Prime Time Promotions.
Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Bwana Sunday Kayuni pia alikuepo kwenye huo mchakato wa kuandaa Soka la Ufukweli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Yale yale kila kitu Simba na Yanga.Hizi klabu zingelekuwa na mafanikio sawa lakini uongozi mbovu,rushwa na hawana hata viwanja vya mazoezi aibu.Hebu badilikeni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...