Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphery Polepole (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa wananchi wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo leo alhamisi Nov.22, 2012. Wajumbe wengine wa Tume, wa kwanza kulia Nassor Mohammed, Maria Kashonda na Riziki Ngwali.
Wananchi wa kijiji cha Mangucha Kata ya Nyanungu Wilaya ya Tarime mkoani Mara wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadlliko ya Katiba leo alhamisi Nov. 22, 2012 katika kijiji hicho.
Wananchi wa Kata ya Mliiba Wilayani Tarime mkoani Mara wakisoma nakala za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na machapisho mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo katika Kata hiyo, leo alhamisi Nov. 22, 2012.
Mkazi wa Kata ya Mliiba, Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Bi. Grace Nyakola (33) akisoma nakala ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha nyepesi wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Kata hiyo, leo alhamisi Nov. 22, 2012.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...