Ndugu yangu Ankal,
 
Salaam sana, najua unayo mambo muhimu ya kuyaweka hapa. Lakini hata hivyo nakuomba unitafutie nafasi ndogo uliyonayo unitolee uwanjani kitu kinachonisumbua kichwani ili wadau wenzangu wanielimishe kwa haya majina.
 
Kuna sehemu Tanzania inaitwa "Mto wa Mbu" huko Arusha na ipo sehemu inayoitwa "Usa River" huko huko Arusha na kuna barabara imefunguliwa na Wakulu wa nchi zetu Tanzania na Kenya inayokuja Namanga Arusha inayoitwa Athi River. Hapo ndipo lilipo tuta linalonitatiza mimi kusonga mbele. Je, majina haya yana uhusiano wowote? Au ni matamshi ya lugha zetu yanayofanana na lugha ya Kiswahili yakasomeka tunavyoyatumia? Maana majina yote hayo yapo Arusha. Nielimisheni ndugu zanguni.
 
Peters Mhoja/Sweden
 petersmhoja@hotmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mto wa Mbu nijuavyo mimi ipo Arusha eneo la Monduli barabara ya kwenda Manyara National Park na Usa River ipo Arusha ukitoke Moshi au KIA ila Athi river ipo Kenya.

    ReplyDelete
  2. mto wa mmbu ipo arusha kabla ya mbuga ya manyara kuelekea Karatu, ngorongoro na serengeti.

    Usa river ni mji mdogo katika barabara ya Moshi Arusha.

    Athi river ni mji ulio kenya

    ReplyDelete
  3. Mtoa mbu na Usa river ziko Arusha ila Adhi river iko Kenya

    ReplyDelete
  4. What is wrong with the names? I don't see any problem.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...