Mwanamuziki nguli wa dansi Barani Afrika, JB Mpiana (mwenye kofia) akiongoza na baadhi ya wenyeji wake pamoja na wanamuziki wa Bendi yake ya Wenge BCBG wakati wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam usiku huu. JB Mpiana na Bendi yake ya Wenge BCBG wanatarajiwa kufanya Onyesho moja kubwa jijini Dar,Novemba 30,2012 kwenye Viwanja vya Leaders,Kinondoni jijini Dar.
Mwanamuziki nguli wa dansi Barani Afrika, JB Mpiana (mwenye kofia) akiongoza na Mwanamuziki mwingine Mkongwe hapa nchini,Ndanda Kosovo (mwenye shati nyeupe) wakati akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam usiku huu.
Mwanamuziki nguli wa dansi Barani Afrika, JB Mpiana akifanya mahojiano na Baadhi ya Waandishi wa Habari waliofika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam usiku huu.





jamani hiyo airport ya uwanja wa ndege wa mwalimu mbona inatia aibu sana angalia kijimlango cha kutokea utasema mlango wa choo mlango mdogoo tena marangi yote kwishinei jamani aibu gani hii mwe!
ReplyDelete