Tunapozungumzia orodha ya wanamuziki waimbaji akimama katika muziki wa dansi wa Tanzania, katika orodha hiyo wapo wengi lakini jina la Dada Tabia Mwanjelwa linajiandika na kujipa nafasi 
katika wanamuziki hao, Mwanamuziki Dada Tabia Mwanjelwa ambaye amewahi kuimbia bendi ya Maquis Du Zaire enzi zile muziki wa dansi ulipokua unatingisha anga kila kona ndani na nje !
na siku za mwisho wa wiki au wikiendi wapenzi wamuziki jijini Dar,wanajimwaga kila kona kwa kupata burudani kamili ya muziki wa dansi ambao ulikua unakamalisha na kuleta maana kamili ya "Furaha ya maisha",Mwanamuziki Dada Tabia Mwanjelwa enzi hizo alikua anatamba na
nyimbo kama vile " Mimi Jane naangaika" na "Kweli maisha ni Safari ndefu" alizoimbia na bendi ya Maquis Du Zaire.
Mwanamuziki Tabia Mwanjelwa ambaye mara kadha alivumishwa kuwa amekufa na baadhi ya wazushi wakati kumbe ukweli Dada Tabia Mwanjelwa bado yupo hai na yupo gado tena Sauti hipo pale pale yaani tajiri wa sauti.Kwa sasa anaendesha maisha yake nchini Ujerumani.
Ni Juzi kati tu alijumuika na watanzania wenzie chini ya Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) mjini Mainaschaff ,Ujerumani na kutoa burudani kiduchu tafadhali tupia jicho video hiyo.

Kama unahitaji mawasiliano tafadhali wasiliana 
na umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...