Na Urban Pulse Creative 
Taswira exclusive ya kumeremeta kwa  Mhe. Naibu balozi wetu wa Uingereza kaka Chabaka Kilumanga na  mchumba wake Irene Joel siku ya jumamosi tarehe 24.11.12 hapa jijini London. 


 Ndugu, jamaa na marafiki kibao  walihudhuria sherehe hii ambayo ilifana sana. Tunapenda kuwatakia kila la kheri katika safari yao mpya walioianza katika maisha ya ndoa. Mungu azidi kuwabariki, 

Asanteni. 

 Maharusi wakivalishana pete baada ya kula viapo
 Dendazzzzz......
 Maharusi wakikabidhiwa cheti cha kumeremeta
  Maharusi wakifungua mziki kwenye mnuso wa kumeremeta kwo
 Maharusi na wanafamilia
 Maharusi katika picha ya pamoja na familia. Kutoka Kulia ni Mama wa Bwana harusi Kilumanga, Maharusi, Mama Irene na Dada wa bwana Harusi Mariam Kilumanga
Mashaaallah...
Mh Chabaka akimlisha mai waifu wake  Irene keki.

Timu nzima ya Globu ya Jamii nayo inatoa pongezi nyingi kwa kaka Chabaka na shemeji Irene kwa siku hii muhimu katika maisha yao. Ukiwa mmoja wa washauri wakuu wetu, na uliye tayari kutusaidia kwa hali na mali, kaka Chabaka, hatuna la kusema. Tumehemewa. Cha zaidi tunakutakia maisha mema na ya fanaka katika ndoa yenu hii...
 - Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Wameremeta kweli, wamepndeza sana. Asante Michuzi, asante Urban Pulse kwa kutuletea uhondo huu. Keep it up ankal! Keep it Urban Pulse!

    ReplyDelete
  2. Congratulations Mhe. Kaka Chabaka & Shemeji Irene. We wish you happiness and good times.

    Marizanga is your time . . . You are NEXT

    ReplyDelete
  3. Hongera sana kwa Harusi !!!

    Kitu kama hiki ni cha kuzingatia sana kwa kuwa wengi wanafikiri Ndoa ni jambo rahisi rahisi tu, inatokea mtu akachukua muda mrefu sana lakini siku ya siku mambo yakawa mambo!

    ReplyDelete
  4. KAKA CHABAKA HONGERA SANA,MUNGU AWAJALIE KILA LA KHERI.MMEPENDEZA SANA NA SASA KAKA KWENYE HAFLA UTAPENDEZA NA MRS.HONGERENI SANA.

    ReplyDelete
  5. Hongera Balozi kwa ndoa!

    Hatumaye tumewakata ngebe wale domo wazi, ohhh Balozi yupo singo, ohhh ana Mchumba tu,

    Nani kawaambia ya kuwa ndoa pekee ndio uadilifu wa mtu?

    Hamuoni watu kibao waliopo ktk ndoa lakini bado ni Vicheche na Wakware kwa saana?

    Kitendo cha Mhe. Raisi JK kumteua Ubalozi ni wazi yeye Mhe.Balozi ni safii na leo habari ndio hiyo!

    ReplyDelete
  6. Hongera! Hongera! Kila kheri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...