Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisalimiana na Viongozi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA),wakati alipofanya ziara katika Kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Leo,kujionea shughuli Mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo. Nyuma ya Waziri wa Uchukuzi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi. Suleiman Suleiman.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(mwenye suti nyeusi) akiangalia eneo la Kipunguni B ambalo lilifanyiwa tathmini kwa ajili ya kuongeza eneo la Kiwanja cha Ndege cha Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba akipata maelezo ya namna kituo cha hali ya Hewa kinavyofanya kazi katika utoaji wa Taarifa mbalimbali za hali ya Hewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kutoka kwa Bi. Pamela Gabriel kutoka Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA).Naibu Waziri wa Uchukuzi alifanya Ziara hiyo kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika Uwanja huo leo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba akipata malezo kutoka kwa Afisa kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), Bw. Elieza Mwalutende, wakati Naibu Waziri huyo alipotemmbelea Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl . Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanja hicho.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(aliyeweka mikono miwili mfukoni) akipata maelezo ya namna kikosi cha zima Moto katika Uwanja wa Ndege wa Mwl Julius Nyerere kinavyofanya kazi,Wakati wa Ziara yake hii leo Katika uwanja Huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege(TAA), Mhandisi Suleiman Suleiman, akisisitiza jambo wakati Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(aliyejishika Kichwa), alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Uchukuzi, Bw. I. Nchasi.
Naibu waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba ,akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA),alipokutana nao leo jijini Dar es Salaam, katika Ziara yake ya kujionea shughuli mbalimbali zinzofanywa katika Uwanja wa Mwl Julius Nyerere.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(wa nane kutoka kulia)akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA), Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) pamoja na wakurugenzi kutoka Wizara ya Uchukuzi. Naibu Waziri wa Uchukuzi amefanya Ziara katika uwanja wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo kujionea shughuli mbalimbali zinazonafaywa katika Uwanja huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. yale yale! angalia heading yako

    ReplyDelete
  2. Uwanja wa JULISU NYERERE upo mkoa gani?

    ReplyDelete
  3. Anonymous said.....
    Hivi wanaangalia na shughuli za wale jamaa wa pale chini kwenye international arrival wanavyosumbua watu na kuwaomba rushwa wanapokuja kutoka nje ya nchi? Nafikiri hili sijui kama waziri analitambua maana hao wafanyakazi wa uwanja wandege upande wa TRA wanatabia ya kugeuza vitambulisho wakati wako pale chini ili usijue majina yao. Wizara inabidi iwashughulikie kama wanavyofanya kushughulikia tatizo la rushwa bandarini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...