Kutokana na maombi ya wadau wengi sana Ankal ameamriwa aweke ngoma moja aipendayo kila siku ili waburudike naye. Basi leo Jumatatu anakuja na ngoma ya Ollie & Jerry ya There's No Stoppin' Us ambayo enzi zao walikuwa wanaimba 'Maiko jakson njooo... sitaaaki. Kama hutaki nendaaaa...' Hii ngoma ilitumika sana kwenye mashindano ya disco ya Break Dance enzi za kina Black Moses, Ommy Sydney, Athumani Digadiga, Abdul Shalamar na wengineo - kwa mnaokumbuka leteni data zaidi....
Home
Unlabelled
Ngoma azipendazo Ankal
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Dancers wa zama zile msimsahau RAY ABDU, Mkali wa kucheza mwenye vituko na mwenye majina mengi.
ReplyDeleteAlikuwa ananyoa nywele mitindo ya ajabu ajabu na kuvaa kiajabu ajabu huku akicheza Muziki kiajabu ajabu.
Nilishuhudia siku moja akitaja majina zaidi ya 32
-RAY MANGA,
-PAKA SHUME
-(,,,mwaga haja ndogo,,,)
-GOLOGOTA
-AWOLOWO
-DZANIMBI
-ADEDEJI
..........na mwengine kibao hadi 32
La ajabu aliambiwa ayarudie kuyataja hakukosea hata moja!
OLD TIME DANCERS LIST:
ReplyDelete.Black Mosses
.Ommy Sydney
.Athumani Digadiga
Wengine ni
.TASS Chiume
.Paylonga (DJ & Dancer)
.Ray Abdu-Adedeji
Acha mambo wewe Pai hakuwa dancer alikuwa brother man tu, ma dancer walikuwa kina Tasi,Digadiga, Mzee Bachu, Ommy Sidney, Abdul Shalamar, Raju, Rumi na Khairoon (baba na mama wa bob junior) na kina black moses. Kama ulikuwa hujafika mjini bado unaweza kuuliza tu au vipi...du kinaa
ReplyDeleteMdau wa 3 anonymous wa Mon Nov 19, 08:38:00 PM 2012
ReplyDeleteKinachochangiwa hapa sio nani ni zaidi, tunachangia kumbukumbu tu!
Kama unaelewa mengi toa mchango wako kistaarabu zaidi ili watu wafaidike...ni hilo tu.
Mtoa maoni wa (3) anony Mon Nov 19, 08:38:00 PM 2012
ReplyDeleteAnawakilisha mamia kwa mamilioni ya Watanzania ambapo mahala pa majadiliano analeta kashfa kejeli na dharau kwa wengine.
Je kwa mwendo huu tutajenga au tutamoboa?
Je, kama Muungwana Muhiddin Issa Michuzi(Mhe.Balozi),Ankali Mwanalibeneke angekuwa na tabia mbovu kama wewe tungetoka kweli?