Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe kuweka jiwe la Msingi ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha leo, Novemba 02, 2012. Kushoto kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kushoto ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila.
Rais Jakaya Kikwete, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha leo, Novemba 02, 2012. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. DMohammed Gharib Bilal. Kulia ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha leo, Novemba 02, 2012. Kulia ni Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.
Rais Jakaya Kikwete, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Makamu wake na Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandera, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Burton Mwamila, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Chuo cha Kikuu cha Nelson Mandera, jijini Arusha leo, Novemba 02, 2012. Picha na OMR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Inatwa Nelson Mandela Institute of Science and Technology ....kwa tafsiri sahihi ni Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela..ila sasa ukiangali kilivyoandikwa hicho kichwa hapo juu...ni aibu afu tunapitisha azimio la Tume ya Kiswahili ya Mashariki mwa Afrika...kweli safari bado tunayo sio tu kwenye English hata kwenye kiswahili.

    ReplyDelete
  2. Hongera JK Unajitahidi kutuwekea mipango bora ya elimu hususan ya sayansi na teknolojia kwa watanzania. Tupia jicho pia elimu ya ufundi satdi iinuliwe zaid naa zaid ili kuleta watu huku juu. Hongera baba JK

    ReplyDelete
  3. Hongera serikali yetu kwa kutekeleza mawazo mazuri muasisi wa uhuru, demokrasia na maendeleo wa bara la africa mzee nelson mandela. Najivunia sana kuwa miongoni mwa watanzania wakwanza kuanza kusoma katika taasisi hii naamini dira na dhima ya chuo hiki kuwa na hadhi ya World class itatimia na kutoa wataalamu wa sayansi na technolojia wenye ujuzi na ueledi wa hali ya juu kwa manufaa ya taifa letu an africa kwa ujumla kwani africa itajengwa na kutatatua matatizo yake na wafrica wenyewe ikiwa uendelezaji wa sayansi na technilojia ni sehemu ya mchakato huo.
    Mungu ibariki Africa
    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  4. Asante sana kaka Michuzi. Kazi yako tunaikubali. Ila kuna makosa ya kiufundi Neno Mandela limeandikwa Mandera sehemu nyingi za picha zako naomba usahihishe maana hata Mzee madiba huko aliko akiona jina lake limekosewa anaweza asifurahie sana.
    Na Taasisi inajitegemea yenyewe yaani taasisi ya kiafrika ya Sayansi na Technolojia ya Nelson Mandela "Nelson Mandela African Institute of Science and Technology" na sio Taasisi ya chuo kikuu cha nelson mandela

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...