Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012 tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012 tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu.Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Kenya,Mh. Batilda - Salha Burhan.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kushoto) akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ismailia Mtukufu Aga Khan (kushoto) katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012.Rais Kikwete yupo nchini Kenya kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu.Wengine Pichani ni Rais wa Kenya,Mh. Mwai Kibaki (katikati) na Rais wa Burundi,Mh. Nkurunzinzah.
Baadhi ya mawaziri na makatibu wakuu wa Tanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa barabara ya Arusha – Namanga – Athi River yenye urefu wa kilometa 104.4 kwa upande wa Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kwenye sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hivi jamani kuuliza sio ujinga na kuelimishwa sio ujinga sasa basi naomba mnijuze

    hiyo ndege ya serikali anayotumia kusafiria mheshimiwa rais ipo moja tu au zaidi ya moja?

    na kama ni moja je zile safari za mawaziri hutumiwa na ndege hiyohiyo au kuna nyingine?

    mfano jana tu raisi wa zanzibar mh dr.shein amerudi kutoka vietnam je alitumia ndege hiyohiyo au kule zanzibar wanayao nyengine ya huko?

    na kama jibu ni hiyohiyo je ina maana wanatumia kwa kupolekezana mmoja anasafiri mwingine anasubiria irudi asafirie nayeye au inakuaje?

    na mwisho namalizia kutoa ushauri kuwepo na ndege japo 2 za safari za kiserikali maana kama ni moja tu itachoka haraka na kusababisha hatari maana haipati muda wa kutosha wa marekebisho.

    ReplyDelete
  2. ndege haipo moja usije kichwa kichwa hapa

    ReplyDelete
  3. Kwa nyongeza kidogo,kwenye picha za Dr.Shein ile ndege ilikuwa na propeller jamii ya Fokker,hii hapa `ya Mramba` ni aina ya Jet.Nadhani zipo mbili tofauti Zanzibar na Jamuhuri ya Muungano(Sina uhakika lakini)

    David V

    ReplyDelete
  4. Serikali Ina Ndege tatu , kale kampya Gulf Stream , Fokker friendship 27 na Fokker 50 ambayo ndo unaiona hapo ni jet lakini Fokker 27 ina propeller engines.. No nimekumbuka hii Fokker 50 ni Ndege ya CCM sio serikali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...