Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua barabara ya Minjingu-Babati-Singida nje kidogo ya mji wa Babati Mkoa wa Manyara. Anayeshuhudia kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji) Dkt Mary Nagu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier wakiweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maeneo ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Frederick Sumaye wakati wa mkutano wa hadhara mjini Katesh mkoani Manyara.
Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Arusha baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maene ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...