MWIMBAJI maarufu wa muziki wa
Injili nchini, Rose Muhando na mwenzake Enock Jonas (Zunguka)
wanatarajiwa kutia chachandu katika tamasha la kwanza kubwa kufanyika
Mkoani Kagera.
Tamasha
hilo la Shangwe Kagera lina lengo la kuielimisha jamii na kuamsha
mwamko wa kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika maisha magumu.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Beula Communications Ltd, ambao ni waandaji wa tamasha
hilo,Melkizedeck Mutta anasema kuwa matayarisho ya tamasha hilo
yanaendelea vizuri kutokana na mwitikio mkubwa wa watu mbalimbali
waliojitokeza kushiriki.
Pia, Mutta anasema bendi ya muziki ya wazawa mkoa huo, Kakau Band pamoja na vikundi vingine vya wanakwaya wa makanisa mbalimbali, kikundi cha watoto yatima wanatarajia pia kutumbuiza.
Mutta anasema tamasha hilo la aina yake linatajiwa kufanyika Uwanja wa Kaitaba na pia kwenye ukumbi wa Lina’s mjini Bukoba, siku ya Uhuru, Desemba 9.
“Mpaka sasa tumekamilisha sehemu kubwa ya matayarisho hayo ikiwamo kulipia uwanja pamoja sehemu ya malipo kwa wasanii ambao watashiriki,” alisema.
Pia,
mkurugenzi huyo aliwaomba wadhamini zaidi na wadau wengine wa maendeleo
na watoto kujitokeza kushiriki ili kuwasaidia jamii hasa watoto yatima
na wengine wanaoishi katika mazingira magumu.
Ni kuhamasisha jamii kuishi kwa amani,kupendana na kusaidia watu wengine hasa wasiojiweza kimaisha ili na wao wajione ni sehemu yao.
Katika kutambua hilo kampuni yetu iliamua kufanya utafiti mdogo nakugundua changamoto nyingi katika Mkoa wa Kagera, mojawapo ni kuwa na watoto
wengi wanaoishi katika mazingira magumu. Baada ya kuliona hili,
tulitembelea vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao, mojawapo ni Tumaini Children’s Centre kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Ki lutheri Tanzania (KKKT).
Kituo hiki kinalea watoto wote bila kujali kabila,jinsia wala dini zao, kwa sasa kituo hiki kinahudumia watoto zaidi ya 800, kwa kuwapatia elimu,chakula, malazi n.k ambapo
kwa muda mrefu kimekuwa kikipata msaada toka Sweden ambao kwa sasa
wametangaza kuusitisha kwa maelezo kuwa jamii ya Watanzania inapaswa
kujifunza na kuanza kuhudumia watu wao wenyewe.
Kutokana na hilo ndiyo maana tumeonelea tuwe na tamasha la kuamasisha jamii ili ianze kuona umuhimu wa kusaidia wenzao wanaohitaji msaada.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...