mmoja wa watoto akiwa amembeba mtoto mwenzake akiomba kupewa chochote kitu kutoka kwa wasamaria wema,kama alivyonaswa na Kamera ya Yetu,eneo la Fire,Morogoro Road jijini Dar.
Pichani
juu ni watoto wakiomba omba chochote kitu eneo la Fire,Morogoro
road,watoto hao wamekuwa wakiongezeka kila kukicha,nadhani imefika
wakati pamoja na kwamba ni watoto wetu na si watoto wa mitaani kama
baadhi ya watu walivyozoea kuwaita,Serikali inapaswa kuingilia kati na
kuchukua hatua za dhati kabisa,kuinusuru hii hali na kuhakikisha Watoto
wetu hawa hawaharibiki wangali wadogo kama waonekanavyo.
Pichani ni baadhi ya wazazi wenye watoto hao wakiwa wamejipumzisha
kimyaa huku watoto wao ndiyo wakifanya kazi ya kuomba omba huku na kule
ili wapate chochote kitu maisha yaendelee.Kiukweli watoto hawa wanapaswa kuhangaikiwa mapema sana kwa maana wana haki ya kulindwa na kuishi kwa amani na upendo kama wengine,Tusipokuwa makini tutajenga Taifa lenye matatizo makubwa.
Akina haki za binadamu wako wapi? Wepesi kuishtaki serikali mbona hawaingilii haya? Au haina maslahi kwao?
ReplyDeleteHaki ya Mungu tena wale waliokataa mimba na kutoroka waangalie vizuri watoto wao wako hapo!
ReplyDeleteMungu atuhurumie.
Mimba zisozotarajiwa.
Mimba zilizokatalia.
Ubakaji.
Umasikini
na Ukosefu wa elimu (sina maana ya litabu hapa) Maana wako walisoma vitabu tu na wameacha watoto barabarani kama hivi! Mkitaka ushahidi mnitafute!
Mungu ibariki Tanzania
In Conservation we say; don't feed the wild animals,because they will keep waiting for you to feed everyday,as a result they will not struggle to find food for themselves.
ReplyDeleteThe same applies to these human being, that's only because they are getting something everyday in this busness, then they will not stop doing it,the only solution is to give them nothing, then if they will face such a situation twice,thrice, or more, consequently they will stop wasting their time.
But so long you give them something, they will not stop waiting for you to give.
Mabilioni ya pesa wanakula NGOs kila mwaka kwa mgongo wa hawa watoto!
ReplyDeletesiyo SWALA bali ni suala.
ReplyDeleteHili jambo la watoto kutangatanga na kuomba kwa kweli linasikitisha.
we anon uliyeandika kwa kiingereza kweli hamnazo...kwani hao watoto unafikiri watafanya kazi gani hapo mjini? ungeongea kuhusu NGO's na wazazi wao kufanya kazi zao ningekuona wa maana lakini kufananisha hao watoto na tabia za wanyama nadhani wewe ndo kama mnyama. usije ukashangaa na wako pia yuko humo. Le Profeseri nini?
ReplyDeleteInasikitisha Serekali isiyojali watu wake..kuna jamaa alitaka kuchukuwa mtoto akamlee Belgium yeye na mkewake lakini mibongo namna ilivo na choyo ilimkatalia pamoja na kuhonga lakini wapi,wanajuwa mtoto akilelewa europ atafanikiwa kielimu and so on!!!wanafurahi kuona hivi...
ReplyDeleteHivi usiku huwa wanalala wapi?bora hata hivyo vidume,lakini hivi vya kike ndivyo viko kwenye hatari zaidi.Miaka 12 tu watu wanaingia.
ReplyDeleteWe Anony, unaemsema huyu aliye andika kwa kiingereza, hivi wewe huwaoni hao mama zao wanapiga story hapo nyuma ya magofu wanasubiri watoto warisk maisha yao kwa kukwepa magari,kwanini hao akina mama zao wasi shughulike hiyokazi ya kuombaomba,kuanza tu kumsema mwenzio bila kuangalia vizuri michuzi anasema nini siyo vizuri.
ReplyDeleteKazi ya kutimiza jukumu hili ni ndogo sana!
ReplyDeleteNi kumkamata Fisadi mmoja kumfilisi halafu pesa yote kuyoka kwake vinafunguliwa vituo vya malezi vya Jamii ili kuwalea.
Sio jukumu la kungoja Wahisani wenye Mashariti magumu kama Uingereza, UN WORLD BANK na IMF.
Ni kupitia ufisilisi huo wa Mafisadi na jitihada zetu binafsi wananchi wa kawaida kuchangia malezi hayo.
Tatizo kubwa ni kuwa tunajua uzazi lakini malezi ahhh jukumu la wengine!
ReplyDelete