Wapenzi wa BBC, ndugu,
jamaa na marafiki,
Tunawaarifu kuwa ibada ya kumuaga ndugu yetu
mpendwa Fred Mtoi, kwa walioko Uingereza itafanyika Jumamosi tarehe Mosi
Disemba 2012 katika Kanisa la St. Anne's Lutheran mjini London kuanzia saa tano
kamili asubuhi.
Anwani ya Kanisa ni:
St Anne's Lutheran Church,
Gresham Street,
London
EC2V
Safari ya kuupeleka mwili wa marehemu Dar es
salaam nchini Tanzania itakuwa Jumatatu tarehe 3 Disemba 2012 jioni kwa ndege
ya Shirika la British Airways na kuwasili huko Jumanne saa moja asubuhi katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Shukran za dhati kwa Shirika la BBC kwa
kushughulikia na kugharamia mipango yote ya kuusafirisha mwili wa marehemu Fred
hadi Tanzania.
Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kadri
zinavyojitokeza kuhusu mipango ya msiba huu mpaka mwili utakaposafirishwa
kwenda nyumbani Tanzania.
Idhaa ya Kiswahili ya BBC
Kwa maelezo zaidi wasiliana
na Zawadi Machibya +44 795 260
7038



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...