Tamasha la Mitikisiko ya Pwani lilianza mwaka 2004 katika ukumbi wa Traventine, mwaka 2008 lilifanyika Msasani club, mwaka 2009 likafanyika P.T.A. Hall iliyoko ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere Kilwa road, mwaka 2010 likafanyika Diamond Jubilee Hall na mwaka 2011 likafanyika tena P.T.A. Hall.
Mwaka huu 2012, tamasha la Mitikisiko ya Pwani linafanyika ukumbi wa Dar Live tarehe 3/11/2012 siku ya Jumamosi. Tamasha litafungua milango saa nne asubuhi. Awamu hii itakuwa ni kwa watoto na watu wazima ambao ambao wako mbali na jiji au wale ambao hawana rukhsa kutembea usiku. Na kiingilio kwa awamu hii ni shilingi 5,000/= kwa wakubwa na watoto shilingi 3,000/=, watapata burudani kutoka katika kundi maarufu la Wanne Star.
Awamu ya pili itaanza saa mbili usiku hadi majogoo kwa kiingilio cha shilingi 10,000 tu. Awamu hii itapata burudani kutoka kwa bendi zipatazo 13 za taarab ambazo ni Diamond Taarab Kutoka Zanzibar, Manuari, T.Moto, Zanzibar Njema, New Zanzibar Modern Taarab, Kings Modern, East Africa Melody, Dar Modern Taarab, Coast Modern Taarab, Five Star Modern Taarab, Jahazi Modern, Mashauzi Classic na Bibie Khadija Kopa, WAUTAKAAA! KIAFRIKA ZAIDI….!



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...