Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania New York na Vitongoji vyake, NYTC (Board na Executive Committee), wanafurahi kuwaalika Watanzania wote wanaoishi New York na Vitongoji vyake, kwenye sherehe ya kuwakaribisha Balozi Manongi na Naibu wake Ndugu Mwinyi, viongozi wapya wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa New York, pia kumshukuru Dr. Seruhere aliyekuwa Naibu Balozi wa muda na Mlezi wa NYTC.
Sherehe hii itafanyika Jumamosi, tarehe 1 December kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 6 usiku kwenye ukumbi wa:
Holy Trinity Greek Orthodox Church
10 Mill Road
New Rochelle, NY 10804
Wote mnakaribishwa.
Tunaomba mchango wa dola 25 kutoka kwa kila mtu, na wanafunzi dola 10 kwa ajili ya gharama ya shughuli nzima. Huu mchango upelekwe kwa wafuatao kabla ya terehe 20 November 2012, Receipts za mchango zitatolewa .
Miriam Abu
Amir Kius
Catherine Kyauka
Shabani Mseba (347( 712-8539
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati.
Uongozi wa NYTC.
Nakumbuka Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuja alianzisha mfuko na zilichangwa pesa zisizopungua dola 10,000 hivi zile hela ziko wapi na mahesabu yake ni nini hasa? Haya mambo ya kuchangishana kwa vitu vidogovidogo acheni. Leteni zile pesa tuzitumie....!!
ReplyDelete