Hatimaye watanzania wamepata mtandao mpya wa kijamii unaojulikana kama mambopoint ambapo watumiaji watakuwa na uwezo wa Ku-chat na marafiki, kualika marafiki, kuona mambo yote yanayoburudisha kwenye mitandao ya kijamii kama facebook.

Hii ina maana watumiaji wanaweza kushirikishana matukio kwa picha (photo sharings), video na maandishi sambamba na kutoa comments kwenye matukio ya watu wengine na marafiki wakati kule kwenda zaidi ya mambo ya kijamii na kuongeza manufaa ya kiuchumi likiwa jambo linaloutofautisha mtandao huo na mingine.

Masoud Mahundi ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Maaarifa Informatics Ltd, wabunifu na waendeshaji wa mtandao wa mambopoint, amesema kuwa mtandao huo unapatikana kupitia tovuti www.mambopoint.com

Mahundi aliongeza kuwa tayari huduma muhimu ya kutangaza kazi imekwisha anza na takriban nafasi 50 za kazi huingizwa kila siku, kutoka idara mbali mbali ndani na nje ya nchi hivyo kuufanya mtandao huo kuwa wa kijamii na kiuchumi.

“Kwa hivyo badala ya kijana kutumia shilingi 800 kununua gazeti, kutafuta kazi kwenye mitandao mingine na kuchati kwingine, sasa atapata vyote katika mtandao wa mambopoint” alisema.

Mambopoint.com ilianza kusukwa tangu mwaka jana, 2011 na wataalam wa IT na ICT wengi wakitokea chuo kikuu cha Dar es Salaam kiasi cha kuutofautisha mtandao huo na mingine kwa kuongeza huduma za kiuchumi na hivyo kuwa social-economic network pekee nchini na pengine duniani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. This is nice kwa kweli ...nimeipenda sana

    ReplyDelete
  2. interesting......hembu tuone kunani huko?!

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli, nawatakia kila la heri mambopoint katika utenda kazi wao. ni jambo la kujivunia kuona kuwa vijana wa kitanzania wanaanzisha vitu vya maana kama hivi. Bravo mambopoint team!

    ReplyDelete
  4. Watanzania tufanye kazi kwa vitendo! chat chat chat chat!

    ReplyDelete
  5. BADO KIDOGO WAJITAHIDI ZAIDI...maana inabd watuvutie kwa vitu vipya ili waweze kututoa kwenye mitandao mikubwa inayo julikana duniani kote...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...