Wafanyabishara wadogo wadogo wanahitajika katika mahojiano ya utafiti (research interviews). Yafuatayo ni maelezo ya ziada juu ya msaada huu:
·         Muhusika atakuwa anajishughulisha na kuwapigia simu washiriki (participants) na pia kupanga ratiba ya mahojiano.
·         Kazi hii inaweza kufanyikia nyumbani.
·         Itahusisha wahusika toka katika wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam (yaani; Ilala, Kinondoni, na Temeke).
·         Mahojiano haya yanatarajiwa kuwa ya mwezi moja kuanzaia wiki lijalo.
·         Malipo ni maelewano.
·         Utafiti huu ni wa kiwango cha PhD.
·         Washiriki ni wamiliki au maafisa wa biashara ndogo ndogo na za kati (owners of small and medium-size enterprises).
Sifa za muombaji
·         Muombaji awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi.
·         Awe anaelewa maeneo mbalimbali ya jiji la DSM kwaajili ya kupanga mahali pa kufanyia mahojiano.
·         Awe na uwezo wa kuandika na kuonge lugha ya kiingereza kama itahitajika.
·         Awe na uwezo wa kufanya kazi bila ya kusimamiwa (being able to work independently).
·         Awe na uwezo mkubwa wa kuwashawishi washiriki (convincing power).
Kama unaona unazo sifa na uwezo wa kazi hii, 
basi wasiliana nami kwa kutumia email ifuatayo:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...