Na Profesa Mbele

Leo nimejipatia kitabu kiitwacho The Great Theft: Wrestling Islam From the Extremists. Mwandishi ni Khaled Abou El Fadl, profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha California, Los Angeles, ambaye kwenye jalada nyuma ya kitabu, ametajwa kuwa "one of the world's preeminent Islamic scholars and an accomplished Islamic jurist."

Nikitafsiri kwa ki-Swahili, ni kwamba mwandishi huyu ni mmoja wa wataalam wa u-Islam ambao wanaongoza hapa duniani na pia ni mwanasheria mahiri wa sheria za ki-Islam. Nimeanza kukisoma kitabu hiki leo hii. Tayari ninaona kuwa hiki kitabu ni moto wa kuotea mbali, kwa jinsi kinavyouelezea na kuutafsiri u-Islam kwa mujibu wa misahafu yake, na kwa jinsi kinavyowabomoa hao wanaoitwa wa-Islam wenye siasa kali. Mwandishi anawabainisha kuwa ni wapotoshaji, kwenye masuala kama nafasi ya wanawake katika u-Islam, jihad, haki za binadamu, ugaidi, na vita.

Kitabu hiki kinanikumbusha kitabu changu kingine, kiitwacho Muhammad: A Biography of the Prophet, ambacho nilikifurahia sana, nikakitaja katika blogu hii. Yeyote anayetaka kujielimisha kuhusu Mtume Muhammad S.A.W. ni vema akasoma kitabu hiki, ambacho gazeti la Muslim News lilikisifu kwamba kinaondoa umbumbumbu uliopo, na ni kitabu muhimu kwa wasio wa-Islam na wa-Islam pia.

Basi nimeona kuwa kitabu cha The Great Theft ni kimoja kati ya hivi vitabu vinavyofafanua kwa umahiri mkubwa ukweli kuhusu u-Islam, tofauti na yale yanayosemwa na hao wanaoitwa wa-Islam wenye siasa kali, ambao wameuteka nyara na wanaupotosha u-Islam. Ushauri wangu ni kuwa tuvisome vitabu hivi. Lakini je, kwa wa-Tanzania, ambao kwwa ujumla ni wavivu wa kujifunza lugha mbali mbali na ni wavivu wa kusoma vitabu, elimu hii itawafikia?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Msicheke, ila si watanzania ni mabingwa wa kusoma picha na kujifanya tunajuwa kila kitu wakati we have no idea. Kwa Tanzania, hivi vitabu haviuziki, mtu ataona bora akanunue kanda ya fleva isiyokuwa na ujumbe wowote muhimu kwake lakini kitu cha maana kama hiki hawezi kununua kwani anaona dhambi kusoma. Michuzi, wewe una tabia ya kusoma vitabu kweli wewe?

    ReplyDelete
  2. Professor Mbele
    Kwa wale ambao sio wavivu wa kujifunza lugha mbali mbali, tumia nafasi hii kutafsiri kitabu au vitabu ili sisi tusiweza hizi lugha tuweze nufaika pia. Nadhani usomi wapo utapatikana kwenye kazi unayofanya kwa jamii yako na sio vyeti ukutani. Wachina hawaongei kingereza lakini wasomi wao wanaoelewa kingereza au lugha mbali mbali kama ulivyotaja wewe, huwa wanatafsiri vitu visomeke kichina kwa manufaa ya jamii nzima. tuache kuona Watanzania kama wamelala tujitanzame wenyewe hasa wasomi wa Kitanzania kuwa ndio wanao angusha jamii zao.
    Binafsi nitashukuru kama utatusaidia na sisi tukaweza soma hivi vitabu vya kiswahili, najua ni kazi kubwa inahusisha vitu vingi ikiwepo na pesa lakini ndio maana wakakuita Professor sio wa kuona wengine hawajasoma bali mtaalamu wa mambo yako ulio na upeo mkubwa kuliko sisi wengine utaweza tumia utalaamu huo kutusogezea maarifa ili nasi kwa uwezo wetu na nyenzo zetu tuweze kujisaidia katika mazingira yetu na kwenye utandawazi. Asante.

    ReplyDelete
  3. I guess there is an extreme molestation of civil rights of human being in every religion,

    The worst of those purported by Catholics orders, I mean the top priests, cardinals, ministers and other so called spiritual and guidance leaders... and that the worst extreme, and crime against human civility..

    I guess you should author one. Mr. Mbele

    http://en.wikipedia.org/wiki/Catholic_sex_abuse_cases

    Hey, what about Evengelical rights in US.. they all pray on the cross.. you should bring the books on Michuzi as well..

    Hey, what about the worst education discrimination right here in Tanzania by the governing Elite of president Nyerere against any other religion... ie Anglican, Methodists, Islam and others...

    Do you remember he shut down all religious schools except Catholics, I guess you benefited immensely Mr. Mbele you dont want to talk about it..

    Thats another extreme of you.!

    ReplyDelete
  4. Profesa Mbele!
    Utakuwa hujaitendea haki Biography ya Mtume Muhammad SAW kama hujakitafsiri au kukisoma kitabu kiitwacho the SEALED NECTAR kilichoandikwa na Saifur-Rahman al-Mubarakpuri.
    Kina jibu maswali mengi sana kuhusu Historia ya Uislamu,mtume n.k

    ReplyDelete
  5. Professor Mbele,

    what exactly do you mean by 'MISAHAFU YAKE'?

    1. Kwenye Usialm Msahafu ni mmoja tuu.

    2. Nashauri watu wangeanza kusoma kitabu kilichoandikwa na John Esposito kinachoitwa 'What Everyone Needs to Know about Islam'

    3. Na kabla hawajafika kwa Esposito why not wasianze kwa kusoma kitabu kinachoitwa MILESTONES kilichoandikwa na Sayyid Qutub ambaye naweza kusema kuwa ni baba wa modern day radical Islamic thinkers na mabaye alibadilisha kwa kiasi kikubwa Muslim Brotherhood iliyoanzishwa na akina Hassan El Banna kule Egypt miaka 80 iliyopita na leo wamechukua nchi.


    Professa Mbele, mimi kwa ushauri wangu naona bora ungetafsiri MILESTONES kbla hujafika huko kwingine.


    Wako kwenye elimu:

    - Wimbi la Mbele

    ReplyDelete
  6. Pia kasome na iweke kwa vigelegele article ya Marehemu Prof Haroub Othman Miraj alivyochambua terrorism na mwanzo wake na wahusika wake wakuu, hakuna Islamic extremism ila ni namna watu wanavyotafsiri na kufuata dini yao, wengine wanachangaya taratibu zao na dini na hii ipo kwenye kila dini na nyingine ni more extreme kuliko uislam lakini havitajwi. Kama wale wanaoona wana haki kuliko wengine mpaka viongozi wao kuingilia maamuzi ya serikali na pia kuitaka serikali kunyamazisha madai ya haki ya waumini wa dini nyingine.

    ReplyDelete
  7. Pia tunaomba mtuwekee kitabu kiitwacho Sinod of Africa (1988) na kile cha Muadhama Cardinal Pengo kiitwacho Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwenye vijiliaSinodi ya Maaskofu waAfrika kwa ajili ya Afrika

    ReplyDelete
  8. Ahsante Kaka Michuzi kwa kutujuza..Ingawa siku nyingine ukitoa mchango wa mawazo unahusu dini..usiandike jina umepata wapi habari..andika tu source toka sehemu fulani..

    Kwani baadhi yetu kabla hatujaona faida ya mchango tunaangalia jina aliyetoa na kutoa hukumu hapo hapo..kuna comment hapo juu utaona kama mtu ameona aliyeleta habari hastahili na anarusha dongo..lini tutaacha kasumba hizi potofu?

    ReplyDelete
  9. Why THIS Book?
    Mbele ana INTEREST gani kwa kutuletea kitabu hiki?
    Is he really concerden about Islam?
    Kuna mamilioni ya vitabu yanayozungumzia uislam na hatuhitaji Mbele atuambie kitabu gani chakusoma khs uislam hasa ukizingatia Mbele si muislam na kadri atakavyojifanya anajua lkn kiuhalisia hajui chocchote khs Uislam sahih.Inshort mm namshangaa sna huyu the so called Prof.Mbele for sure mtu mwenye busara hawezi kujiingiza kny sensitive issue km hii hasa ukizingatia kwamba yeye si katika wahusika wakuu wa Dini husika.

    ReplyDelete
  10. Wewe anony wa Sat Nov 10, 10:15:00 AM 2012, ulishafundishwa kulipiza visasi ndo mana hoja imewekwa kuhusu wanaoitwa waislamu wenye siasa kali, wewe unaleta mambo ya ukatoliki Tanzania. Kukufahamisha tu ni kwamba wakati wa nyerere shule za wakatoliki nyingi zilitaifishwa mfano PUGU, FORODHANI na zingine nyingi mikoani. Shule ambazo hazikuitaifishwa ni zile zilizokuwa zinafundisha upadri. Sasa ulitarajia upadri ufundishwe chuo kikuu DSM au ufundishwe Azania Secondari? Mbona madrasa zenu hazikutaifishwa na huziongelei? Atahari za kufundishwa kulipiza visasi ndizo zinawatafuna. Kila kitu mnakitazama kwa kuangalia wenzenu wanafanya nini badala ya kuangalia umuhimu wa hicho kitu kwenu.

    ReplyDelete
  11. Pro maliza kusoma kitabu kwanza ndio useme .
    Halafu unaposema misahafu yake maana yake ni nn? kwani kuna misahafu mingapi? Au mwenzeui msahafu ni nini kabla hujaandika fanya utafiti kwanza.
    Msahafu ni mmoja tu na uliandikwa tangu wakati wa Mtume(saw) kwahiyo huyo alie andika hawezi kuwa na misahafu yake.

    ReplyDelete
  12. Kama profesa umesona vitabu vingi na ungependa kutoa mchango nchini kwako, andika kitabu chako.

    Kuanzisha mijadala kama hii kwa mambo yanayohusu DINI, kwa uzoefu wangu, HAKUNA TIJA.Utaishia kutukanwa tu (labda michuzi akusaidie kubana hizo comments).

    Vile vile use makini na vitabu vya maprofesa wa marekani. Hivyo vitabu unavyosifia UKICHUNGUZA utakuta KUNA VITABU VINGINE VYA WANAZUONI WALIOANDIKA KUVIPINGA - Kwa hiyo usichukue elimu ya vitabu viwili FOR GRANTED.

    Kumbuka, dini ni imani na si analysis tu na ndio maana WATU WANAJITOLEA KUFA, WANAMWAGIANA TINDIKALI, nk. ImanI ni metaphisical, ni vigumu kui-analyze kwa mtazamo wako wewe wa ki profesa kwamba usome hiki na kile then upate jibu!!!

    ReplyDelete
  13. Sidhani kama hoja ya "UISLAMU" ina uhusiano wowote na mambo ya NYERERE. Hapa kinachozungumziwa ni IMANI ya kiislamu GLOBALLY, si matatizo ya wakristo na waislamu Tanzania!!!

    Msiyumbishe mjadala kwa kuanza kujadili matatizo ya wakristo na waislamu TANZANIA!!!

    ReplyDelete
  14. michuzi kwa kutupa ubrudani. MIMI NDIO MANA NASEMA WANAOJIITA MAProf kwa dini ya leo ni sawasawa na mkulima wa busara wa enzi ya babu yangu.

    ReplyDelete

  15. Prof. Mbele.

    Kabla hujahamasisha waTZ kusoma siasa kali, hebu hamasisha waTZ kuelewa kinachotuzunguka.

    Hamasisha usomaji wa kitabu 'Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953- 1985, by John Sivalon (1992)

    Hapa ndio tuchambue na tujue hii Siasa Kali maana yake ni nini, na ni nani anayestahili kuitwa hivyo,

    Kama Anon wa 3 alivyogusia.

    ReplyDelete

  16. HAKUNA KITU KAMA "MISAHAFU YAKE"

    MSAHAFU UKO MMOJA TU, SAHIHISHA, WEKA "MSAHAFU WAKE"

    ReplyDelete
  17. Anon wa 03:55:00 PM.

    KABLA HATUJAPEPEKANA MBALI KOTE HUKO, KWANZA KIELEWEKE HAPA NYUMBANI, TUNAJAZWA HEWA CHAFU NYINGI SANA NA HAWA WASOMI AMBAO BAADHI NI WAPOTOSHAJI.

    HIVYO BASI,
    KWANZA KAMA KWELI TUNATAKIANA MEMA KWENYE KUSOMA, DIRECT US TO THOSE LEAST KNOWN AREAS IMMEDIATE TO US NDIO "MKATUELEWESHE" MAMBO YA HUKO KWENGINE.

    ReplyDelete
  18. Vipi Profesa Mbele? ulikuwa unafikiri hii itakutoa nini?

    ReplyDelete
  19. hii imebackfire spectacularly

    kwa nini asitafsiri kitabu kilichoandikwa na HAMZA NJOZI kinachoitwa MUSLIM & THE STATE?

    ReplyDelete
  20. Profesa pole jamaa namjua Huyo amesema quran imekosewa na yeye kafiri wa kutupwa. tizama vedio ya zakir naik na Profesa William kwenye maswali na majibu utapata Habari zake.

    ReplyDelete
  21. University of California Los Angeles (UCLA) is a State University. Na shaka (kwa kulinda ajira na kupendezesha profile) profesa wake anaweza kutoa ukweli unao onekana kama incriminating au usio - sound good - kwa American au Western audience. Na vile vile kitabu lazima kiuzike.

    ReplyDelete
  22. Bwana Mbele utaacha lini kuuandama Uislam? Unajifanya wewe ni mchambuzi sana wa vitabu na msomi uliebobea, in fact wewe ni mdini uliebobea. Hivi unafikiri waIslam hawaijui dini yao ila kwa maelezo yanaondikwa na hao so called Islamic scholars? Watu wanapigania haki zao mnawaita extremist, fundamentalist, terrorists. Ujue hata Mandela alitwa vyote hivyo hadi justice ilivyo prevail, acheni hizo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...