Baadhi ya wahitimu wa chuo kikuu cha Dodoma wakiwa kwenye foleni tayari kwa kuchukua majoho yao ambayo watayavaa katika sherehe za kumalizia safari yao ya miaka mitatu ya masomo yao ya Chuo Kikuu Cha Dodoma hapo Jana na leo
Foleni ikiwa haisogei kabisa huku wengine wakiendelea kusubiri na wengine kupiga stori mara baada ya kutokuonana takribani miezi minne tokea walipomaliza masomo yao chuoni hapo
Wahitimu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma UDOM kitivo cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha wakiwa kwenye foleni ya kuchukua majoho tayari kwa kuhudhuria sherehe za mahafali ya tatu ya chuo kikuu cha Dodoma yanayotarajia kufanyika tarehe 21 na 22 Novemba 2012 katika viwanja vya Chimwaga 
Hapo mwenye nguvu ndie alikuwa wa kwanza kuingia na mnyonge alisubiri yote hiyo wakigombania kuingia wa kwanza kwaajili ya kuchukua majoho tu
 Huku wengine wakiwa wamejikalia zao chini wakisubiri vurugu za kuingia kwaajili ya kuchukua majoho ziishe nao waingie kuchukua majoho yao
Baadhi ya wahitimu mara baada ya kuchukua majoho yao tayari kwaajili ya sherehe za mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu cha Dodoma yanayotarajiwa kufanyika tarehe 21 na 22 novemba 2012 katika viwanja vya Chimwaga Chuoni hapo
 Mara Baada ya Kuchukua Majoho yao Wahitimu hawa waliyajaribu kwanza kuona yanawatosha huku wengine wakisema kuwa "safari hii Majoho Yanatolewa Kwa GPA likikuenea GPA yako ni kubwa lisipokuenea GPA Yako ni Ndogo". Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hivi hadi lini ustaarabu utaingia huko Tanzania? Kimewashinda nini kupanga mstari na kuchukua hayo majoho? Kupanga tu mstari kunawashinda na tunaamini hawa ni wasomi, je wale wasio wasomo na wenye hekima itakuwaje? Jamani mnapaswa muonyeshe ukomavu wa kufikiri, ninyi sasa ni watu wazima wa kutosha na wengine wenu watakuwa viongozi wetu, acheni ubinafsi fuateni sheria. Kupanga mstari na kusubiri zamu yako ni ustaarabu....tunajiabisha mbele ya watu wa mataifa mengine.

    ReplyDelete
  2. hivi vyuo vikuu kama hii bado nikugombea majoho kwenye umri kama huu. Hamna hata nidhamu???mungu atupe akili.

    ReplyDelete
  3. Wana graduate mengine Lakini Ustaarabu hawajafundishwa , Sijui watu wataacha lini u selfish,Kila mahala Mpaka wasukumane serikali inatakiwa kuangalia swala hili wafungue vituo vya kufundisha watu Ustaarabu na kuacha kuwa wabinafsi lasivyo tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu. Au wawaoneshe watu sinema za bure jinsi nchi zingine walivyo wastaarabu Hata chooni wanapanga foleni Hata kwenye basi Kuna foleni. Hebu walete hao ulaya halafu akute watu wamepanga foleni ya kupanda basi awapite watu Wengine.watamuona hana akili Au mgonjwa. Kwa hiyo tustaarabike Najua itachukua miaka mingi saaaaana. Aibu saaaana.

    ReplyDelete
  4. Wanavyo banana na kusukumana mlangoni utadhani Wameambiwa majoho hayatoshi. Hata kwenye mabasi Ni hivyo hivyo unakuta mtu anatiket yake Lakini Lazima apiganie mlangoni kwanza Mpaka shati lichanike. Yani Kuna UBINAFSI wa hali juu sana Kwa wa tz Sijui utakwisha lini. Nimewahi kusafiri na kukaa siti moja na mbongo kwenye KLM ukimuona kavaa suti katikati ya Mimi na yy kulikuwa na mzungu Akaanza kuongea naye baada ya muda kidogo Akaanza sifa zake or mm Nina degree ya kitu fulani Nina fanya kazifulani mzungu anaitikia tu nani kamuuliza? Kidogo akaja dada anagawa snack Ana biskuti na pipi pipi na choclate aliipofika Kwa huyu kaka jamaa akachukua mfuko wa karatasi kwenye mfuko wa kiti cha Ndege hiyo mifuko kawaida huwekewa taka taka za ziada Yule dada akamuuliza kama anataka kitu chochote kwenye hiyo basket Huku akimwekea basket karibu yake mbongo alivyo selfish akachukua nyingi Akaanza kuja ule mfuko niliona Aibu kiasi kwamba Yule dada aliponiuliza Mimi kama nata nikasema Asante mm sitaki Sasa Ustaarabu uko wapi.

    ReplyDelete
  5. Haya ingine Hii July nilisafiri na pricsion kwenda mwanza dada moja kakaa karibu yangu anaonekana mstaarabu alikuwa kakaa dirishani hakunisemesha baada ya muda nikawa naongea na jamaa moja upande wa pili karibu yangu tukaletewa sandwich na kulikuwa na vipande viwili vya bisct Yule dada kala kamaliza akaniuliza unakula hiyo Yani biscut nikamuuliza unataka akasema ndio nikampa nikawanaendelea kuchat na Yule kaka karibu yangu. Yule dada akanigusa mabega nikamtazama Akaniambia Muulize Huyo kaka kama hali hizo biscut anipe niliona nooma sikuweza hata kumuuliza ila nilimwambia yule kaka unasemeshwa yule dada akamwambia naomba hizo biscut jamaa akampa.Sasa jamani Ustaarabu uko wapiiiii

    ReplyDelete
  6. nyie acheni hizo kwani kuwa majuu ndo usatarabu?? tuache na TZ yetu ndo ilivyo munashangaa nini???

    ReplyDelete
  7. Acha ujinga ww nani kakuambia kukaa nje ndo ustaraabu ukweli unauma ss wa bongo sio wastaarabu kbsa yaani tunatia aibu sana hata kenya wanatupita ss ona hao wanafunzi wanavyogombea kuingia ndani eti ni wahitimu wa degree miaka 3 ushezi ni aibu ndo maana wakenya wanachukua kazi zetu then tunalalamika sio wastaarabu ndo maana form four iyo ni one of cretaria employer anangaalia tubadilike jamani

    ReplyDelete
  8. Anonym wa Wed Nov 21, 10:47:00 AM 2012. Naomba fursa hii nikujibu swali lako: Kuwa majuu siyo ustaarabu. Lakini ustaarabu ni upo majuu...katika kiwango kikubwa ambapo si lazima uambiwe...utauona tu mwenyewe. Na hata hiyo mifano kadhaa iliyotolewa hapo juu itakuambia kuwa kweli kuna ukosefu wa ustaarabu. Hata mimi mwenyewe nilipoona hiyo picha ya watu wanaohitimu chuo kikuu wanavyong'ang'ana mlangoni nilianza kujiuliza, hawa ndio wanaohitimu au wamewatuma vibaka fulani kuwachukulia majoho yao? Ni kweli tunahitaji kubadilika ili kuweza kuendana na huu utandawazi. Haiwezekani kuwa na tabia ya mtanzania tu ambayo ni mbaya au nzuri na kujidai kuwa mambo yatakwenda vizuri tu...ndiyo maana tunaendesha magari ya kijapani, pikipiki za kichina, miswaki ya india, taulo za kitanzania, mashati ya kimarekani, suruali za Africa kusini, vijilo vya china, sufuria za Ujerumani nk...ni kwa sababu tunahitaji ustaarabu wa mahali kwingine ili kuweza kukidhi haja zetu. Hali kadhalika tunahitaji kuiga tabia zilizo njema kutoka sehemu nyingine ili kurahisisha maisha ya kila siku.
    Barikiweni watanzania wote...tuige tabia njema..na pale tunapokosolewa, tukubali na kujirekebisha.

    ReplyDelete
  9. Huyu jamaa Wed Nov 21, 10:47:00 AM 2012.
    Yani bila aibu anasema aachwe, yani anaona kuwa ni ujanja kusukumana mlangoni, tena msimi wa chuo kikuu.
    Hao kesho ndio viongozi unafikri watakuwa na ustraabu wa kufanya maamuzi ya busara au watagombania pesa tu na kuangamiza wasio na nguvu za kugombana?
    Ndugu hiyo niaibu sana kwa msomi wa chuo kikuu kama wewe, hata mimi ni Mbongo ila sifagilii huo ujinga.

    MUNGU tupe busara watoto wako

    ReplyDelete
  10. Ubinafsi na kusukumana kwa hawa wasomi ni dalili tosha wakipewa uongozi wataanza kufuja mali za umma kwa ufisadi na ulafi.

    Kweli inabidi somo la civic lihusishe pia na uwajibikaji, kujali wengine na ustaarabu kwa jumla ili wasije kuwa mafisadi kwa uchu wa kupata wao tu.
    Mdau
    Havard Univ.

    ReplyDelete
  11. nchi ya ujamaa bwana wako huru........

    ReplyDelete
  12. Hahahahaha!

    Niacheni nicheke,

    Mwanasayansi Nguli duniani Albert Einstein mwaka 1947 aliwahi kutoa maneno akisema ''I fear the day when you will see the use of technology is exceeding in life applications and mankind assumpitions are applied everywhere''....yaani ''NAOGOPA ITAKAPOFIKA SIKU TEKINOLOJIA INAPITILIZA KATIKA MAISHA YA WATU NA WATU KUTUMIA UAINISHAJI WA KISAYANSI KTK KILA KITU CHA MAISHA YAO''

    Wasomi mmetoa kali ya mwaka, ni kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya ukubwa wa maumbile ya mwili wako na uwezo wako kimasomo yaani GPA (Grade Point Average)!

    ReplyDelete
  13. Je, kukiwa na Joto itakuwaje na Majoho hayo?

    Kwa nini tusizingatie hali ya hewa na Ukanda wa Kijiografia kwa nchi yetu?

    Kwa nini badala ya Majoho wasivae Migolole?

    ReplyDelete
  14. Mdau wa 13 juu anony Thu Nov 22, 11:02:00 AM 2012

    Jamaa hawawezi kuvaa Migolole kwa kuwa kwenye picha watakazopiga za kumbukumbu wataonekana Washamba kama vile wapo Jandoni au Unyagoni, kwao itakuwa soo !

    ReplyDelete
  15. Mdau wa Thu Nov 22, 11:02:00 AM 2012

    Hawa madogo mabishoo sana hata kwa mtutu wa bunduki hakuna atakayekubali kuvaa Mgolole kwenye Graduation!

    Kama Mdau mmoja hapo juu anavyochangia akisema hawa wapo ktk Kizazi cha UBINAFSI, UCHU WA MADARAKA NA MALI na UFISADI uliopindukia sio rahisi wakauenzi Utamaduni wa Mtanzania kwa kuvaa Migolole!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...