Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo akiwa pamoja na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Bw. Klaus-Peter Brandes mara alipomtembelea ofisini kwake. Balozi huyo aliongozana na watendaji kutoka kampuni ya Koch Engineering & Construction ya nchini Ujerumani ambao wanania ya kuwekeza katika miradi ya nishati ikiwamo gesi asilia, umeme wa upepo, jua pamoja na kuwekeza katika viwanda vya uzalishaji mbolea.
Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo akimuonesha Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Bw. Klaus-Peter Brandes ramani ya bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mnazi Bay Mtwara na Songosongo hadi Dar es Salaam. Profesa Muhongo alimueleza mheshimiwa Balozi kuwa Serikali ina mpango wa kuzalisha umeme kwa njia ya gesi katika eneo la Somangafungu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Prof.Muhongo hao wameingia kwenye `anga` zako mkuu.Wape NONDO.Mambo ya Karoo sediments..haaa haa.Mungu akupe nguvu na afya njema Prof.

    Mimi mwanafunzi wako UDSM,Geology 19xx

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...