Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Zara Tours,Zainab Ansell akizungumza na Wanahabari mapema leo mchana,Mikocheni jijini Dar kuhusiana na mafanikio waliyoyapata tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo mnamo mwaka 1987 ikiwemo kupata tuzo 2012 Humanitarian,mjini London,Uingereza.Aidha Bi Zainab ameeleza kuwa kupata kwa tuzo hiyo ndani ya kampuni yake ni heshima kubwa kwake pamoja na wadau mbalimbali wa mambo ya utali,aidha ameongeza kuwa kampuni yake itajijengea heshima na kuongeza juhudi kubwa katika suala zima la kuutangaza utalii wa ndani ya nchi hii.kulia ni Meneja Mkuu wa kampuni ya Zara Tours,Leila Ansell.
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Zara Tours,Zainab Ansell alipozungumza nao mapema leo mchana kuhusiana na mambo mbalimbali ya kampuni yake na namna gani ya kuutangaza utalii wa ndani na nje na namna ya kuisaidia jamii katika nyanja mbalimbali.Kwa habari zaidi kuhusiana na Zara Tours bofya; www.zaratours.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...