Tanzania Bunge Sport Club Netball imefanikiwa kuwa kileleni baada ya kuitandika timu ya muungano ya Jumuiya na Bunge la Afrika Mashariki kwa mabao 49-9.
Katika mchezo mkali wa mashindao ya michezo ya mabunge yanayoendelea jijini Nairobi, Kenya, timu ya Tanzania imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuwachakaza bila huruma wenyeji wao Kenya kwa mabao 51-25.
Mashindano haya ambayo huandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Bunge la Afrika Mashariki kwa lengo la kudumisha mshikamano, yanatarajiwa kufikia kilele tarehe 14 Disemba 2012.
Tayari Tanzania imeweka kibindoni mabao 100, mtaji ambo si rahisi kfikiwa na timu nyingine zilizosalia.
Tayari Tanzania Bunge Sports Club Football wameshajihakikishia kuingia nusu fainali baada ya kutoa adhabu kali kwa timu za Kenya na Rwanda. Kwenye mechi yake na Kenya, Tanzania ilijipatia mambo 5-0. Aidha kwenye mchezo wake na Rwanda Tanzania iliifunga Rwanda mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa City.
Awali Kenya Bunge Sports Club Football ilitoka sare ya 1-1 na Afrika Mashariki katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanya wa Nyayo mbele ya Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mh. Margreth Natongo Zziwa ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo.
Aidha kwenye mchezo kati ya Uganda na Afrika Mashariki Uganda ilijipatia mabao 2 -1, huku Rwanda ikijipatia magoli 2-0 dhidi ya Kenya
Timu ya Tanzania.
Timu ya Afrika Mashariki.
Watazamazi wakifuatilia mchezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...