Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (kulia) akimkabidhi mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Waendesha Pikipiki mkoa wa Mwanza Makoye Bunoro Shilingi 50,000/= kwa ajili ya kuweka mafuta katika pikipiki za kitengo cha Polisi jamii pale wanapoenda kupambana na wahalifu.Umoja huo unawasaidia waendesha pikipiki 2034 kupata leseni na mafunzo yaliyotolewa na Chuo cha VETA kwa gharama naafuu.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (kulia) akiongea jambo hivi karibuni na viongozi chama cha Umoja wa wapanda pikipiki wa mkoa wa Mwanza (hawapo pichani) alipowatembelea ofisini kwao eneo la Mlango mmoja ili kuona shughuli zinazofanywa na umoja huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja huo Makoye Bunoro.
Mdhibiti wa mali za chama cha Umoja wa wapanda Pikipiki wa Mkoa wa Mwanza Faraji Abdalah (kushoto) akimwelezea Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (kulia) jinsi umoja huo ulivyoweza kuunda kitengo cha polisi jamii ambacho kinashirikiana na Jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu. Katikati ni Mwenyekiti wa Umoja huo Makoye Bunoro.
Viongozi wa Umoja wa wapanda Pikipiki wa mkoa wa Mwanza wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi (hayupo pichani) akiwaeleza jinsi wanavyoweza kuunda SACCOS yao na kukopa fedha kutoka mfuko wa vijana ambazo zitawasaidia kununua pikipiki zao na kujiajiri wakati alipowatembelea ofisini kwao ili kuona shughuli zinazofanywa na umoja huo.Picha na Anna Nkinda – Maelezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...