Maofisa wa Benki ya CRDB kutoka makao makuu Dar es salaam(Mkurugenzi wa wateja wa kati na wadogo, meneja Mahusiano Tanzanite Akaunti,pamoja na Meneja wa biashara ya kilimo) wako katika ziara ya kikazi nchini Oman kuanzia tarehe 18/12/2012 mpaka 29/12/2012.

Maofisa hao wakiwa huko Oman watafanya mambo mengi yakiwemo;-

1.kukutana na wafanya biashara wa Oman wenye asili yakitanzania na Watanzania kujadili fursa za uwekezaji na kujipatia mahitaji ya huduma za Benki kwenye Biashara zao kupitia CRDB.

2.Kusimamia zoezi lakufungua akaunti za Tanzanite( Akaunti maalumu kwa Watanzania walio nje ya nchi).

3.Pia watauza bidhaa nyingine za CRDB kama kupata huduma za kibenki kupitia mtandao, kupata statement kwa njia a electroniki,Tembocard Visa na Mastercard.

Siku ya Ijumaa tarehe 21/12/2012 watakua ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Oman kuanzia saa tatu asubuhi mpaka mchana kutoa huduma zilizoainishwa hapo juu.

Siku ya Jumamosi tarehe 22/12/2012 watakuwepo katika mkutano na watanzania utakaofanyika Crown Plaza Hotel Muscat kuanzia saa tatu asubuhi.

Kufungua akaunti utatakiwa kuwa na Picha 2, kopi ya hati ya kusafiria pamoja na kianzio chenye thamani ya shilling 20,000 kwa TSH akaunti au USD 50  kwa USD akaunti na fomu za akaunti ya Tanzanite zilizosainiwa.

Kwamaelezo zaidi wasiliana na Meneja Mahusiano Tanzanite akaunti(Mr. Crispin M. Sichalwe) kwa namba ya simu ifuatayo;+96899142025

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...