Jengo la Benki ya CRDB Burundi.
Rais wa Burundi Piere Nkurunziza akiwasili katika sherehe za ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB jijini Bujumbura, Burundi. Benki ya CRDB imekuwa Benki ya kwanza ya kizalendo kufungua tawi lake nchini Burundi.
Rais wa Burundi,Mheshimiwa Piere Nkurunziza akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Benki ya CRDB nchini Burundi.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei.
Raisi wa Burundi Mheshimiwa Piere Nkurunziza akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB Tully Esther Mwambapa alipokuwa akiwasili katika sherehe hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Burundi Dkt. James Nzagi (Kushoto) na Katibu wa Benki hiyo Bwana John Rugambo(2 kushoto) na Meneja Mkuu wa Benki ya CRDB Nchini Burundi Bw. Bruce Mwile.
Raisi wa Burundi Mheshimiwa Piere Nkurunziza akiwa katika ya pamoja na uongozi wa juu wa Benki ya CRDB.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB nchini Burundi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzano kutoka Dar es Salaam.
Jimmy kazi nzuri sana kaka naliona Jengo limetulia sana.
ReplyDeleteKwa kweli hii ni mojawapo ya siku za kujivunia sana kama Mtanzania. Go CRDB, go...
ReplyDeleteCRDB kazi nzuri sana, mmefungua njia, na kampuni nyingine za kizalendo zifuate mkondo huo..mmpetutoa kimasomaso!
ReplyDeleteHongera kwa benki ya CRDB kwa kuvuuka mipaka,hii inaonyesha jinsi gani hii benki inakua kwa kasi ikiwa chini ya uongozi wa Daktari C. Kimei. Nakupongeza sana Dr Kimei kuifikisha benki hapo ilipo kutoka pale ulipoitoa( From loss making to profit making within short time-). Hongereni kwa wafanyakazi wote wa CRDB kwa ushirikiano wenu.
ReplyDeleteHongera Dr. Kimei hongera Tullyesther Mwambapa, hongera team nzima ya CRDB, haya ndiyo tunayoyataka siyo tunaingia kwenye shirikisho la EAST AFRICA wakati hakuna makampuni yetu nchi zilizokwenye shirikisho sasa twende Kenya uganda na rwanda
ReplyDeleteaaahh,mmeangalia hisa za crdb lkn?au mnafurahia majengo tuu na branch nyingi.kwa nini hisa za crdb zipo kwenye danger zone i mean zinadroopkwa kasi sana kuna nini hapo?mlieleweshe jamani wachumi,maana mi niko huku kishumundu nauza mbege tuu sielewii.
ReplyDeleteCRDB-Mnatakiwa sasa muelekeze nguvu zaidi ktk uwekezaji na Masoko ya Hisa hasa ktk asset za Nishati na Madini kama Gas,Oil and Uranium, ni vile neema zote hizi za mali zinazo akisi Ukuzaji wa haraka wa Mitaji na Kifedha (Rapid Financail Growth Asset Classes) tunzazo nchini.
ReplyDeleteSio Muwaachie Wakenya na Mabenki yao wawapige bao kwa kuanzisha wao wakitumia Mlango wa Afrika ya Mashariki!
hivi ni vitu vya kusifiwa kuwekeza nje ya nchi na ndani ya Tanzania..Sio kila siku tunaleta wakezaji wa nje nchini kwetu na muda wa sisi kuwekeza kwa wengine kwa manufaa yetu.I salute... Big up
ReplyDelete