Kwa mapana na marefu hii imekuwa wiki ngumu sana kwangu. Kuona ya kwamba ningali nadunda na nipo hapa nimeketi na kuanza kuandika hiki ninachoandika, ni ushuhuda tosha kwamba Mwenyezi Mungu bado yungali ana madhumuni na maisha yangu! Ni jambo linalotia faraja.

Wakati nawaza na kujaribu kuchagua wimbo wa kuweka katika segment hii ya kila Ijumaa ya Zilipendwa, nilijishtukia nakumbuka baadhi ya mikoa na bendi kutoka katika mikoa hiyo ambayo niliwahi kutembelea na kuishi. Mojawapo ya mikoa hiyo ni Mkoa wa Tabora ambako mpaka leo bado nina ndugu wengi tu. Nakumbuka babu mmoja aliyekuwa akituuzia “mantalali”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Uliponikumbusha babu muuza ntalali nikakumbuka pia wapo wengine wawili. Mjoja alikuwa anauza'asali mbichi'na mwingine 'dagaa wa Kigoma'. Hawa walikuwa wantembeza hizo bidhaa mitaani na kuzitaja kwa sauti kubwa ili wateja wasikie. Yani ilikuwa ni raha tupu.

    ReplyDelete
  2. Mboka baba!, Mboka baba!, Mboka baba!, Mboka baba!,Mboka baba!, Mboka baba!, Mboka baba!, Mboka baba!,Mboka baba!,Mboka baba!

    Tabbora!, Tabbora!, Tabbora!,Tabbora!,Tabbora!, Tabbora!,Tabbora!,Tabbora!,Tabbora!,Tabbora!

    Hapo juu: maneno MBOKA BABA na TABBORA,

    1.MBOKA BABA,
    'Majani pia ni dawa' kwa wale watumiaji wa dihaa hii ambayo ni kosa la Kisheria nchini kwetu unaposema MBOKA BABA wanakuwa wameelewa ni msemo unaoashiria uasilia wa bidhaa hiyo ya 'majani' umetokea Tabora kama inavyojulikana wao kule Isevya wana 'manyasi' makali sana!

    2.TABBORA,
    Lina herufi bb kwa kurudia sio kama nimekosea bali ni vile ndugu zetu Wanyamwezi wanavyolitamka neno TABORA kwa kukazia kulingana na Lafudhi yao ya Kiswahili cha Bara!

    ReplyDelete
  3. Ahhh Rhumba lilikuwa zito sana!

    Je, Mhe. Rage Mbunge wa sasa wa Tabora Mjini huku ukiwa na Bastola yako kiunoni ndani ya Ukumbi wa Dansi uliucheza mziki huu?

    ReplyDelete
  4. Ehhh baba TAWUWOLA!,

    Neno 'tawuwola' lina maana TABORA isipokuwa lineandikwa kutokana na Lafudhi ya matamshi ya Kinyamwezi!

    ReplyDelete
  5. Tabora,the forgotten region of Tanzania,nothing has changed since I have known the place over the past 38 years, so sad.
    Sokoni ni vile vile tu, the railway station is filthy and delapidated, it looks like the ruins,oops two new structures have emerged during this time,Mwinyi stadium and the new bus stand, but economically Tabora is dead and not advancing at all, other Ministers help their regions but not Sitta. I love the place, my mind is imbued with beautiful childhood memories. NTALALI,ZAMBARAU "MIZUMBA",TABORA JAZZ,MATOBOLWA,MAKOPA, NSWALU, NSANSA, MBUGUSWA etc.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...