Diwani wa Kata ya Kipawa,Bonnah Kaluwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza Uzinduzi wa Mradi wa Kuwaendeleza Wanawake na Wasichana wa Kata ya Kipawa kuwa Wajasiliamali na wanaoelewa biashara na Taaluma zao,unaofahamika kama WANAMA (Wamama na Maendeleo).Kulia ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Kipawa,Said Fundi.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Dalring Hair,Edward Shilla (kulia) ambao ni wadhamini wa Mafunzo ya Mradi huo wa WANAMA akizungumzia namna walivyoweza kujitokeza kudhamini Mradi huo utakaowawezesha Wanawake na Wasichana wa Kata ya Kipawa kuwa Wajasiliamali na wanaoelewa biashara na Taaluma zao.Kushoto ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Bonnah Kaluwa ambaye ndie Mratibu mkuu wa Mradi.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kipawa,Said Fundi (kushoto) akitoa shukrani kwa wadhamini wa Mradi wa Kuwaendeleza Wanawake na Wasichana wa Kata ya Kipawa kuwa Wajasiliamali na wanaoelewa biashara na Taaluma zao,unaofahamika kama WANAMA (Wamama na Maendeleo) ambao ni Kampuni ya Dalring Hair.Katikati ni Diwani wa Kata ya Kipawa,Bonnah Kaluwa na kulia ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Dalring Hair,Edward Shilla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...